26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa Afya akagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Geita

MWANDISHI WETU – GEITA

WAZIRI wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefaya ziara katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita unaotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kama Mkandarasi na Mshauri Elekezi.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa mradi huo, alisema kuwaamefurahishwa na kasi ya ujenzi huo unaotekelezwa kwa ubora na TBA.

Alisema hospitali hiyo itakuwa mkombozi katika mkoa huo  kwani itasaidia kuokoa maisha ya wanawake na watoto wengi kutokana na kuwa wamesongezewa huduma karibu na kwamba TBA imefanya kazi nzuri kutokana na kuwa mradi unaonekana unaendelea vizuri.

“Pia namshukuru sana Mhe. Rais Dk John Pombe Magufuli kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu na miradi mingine ya Afya kote Nchini.

“Vile vile nampongeza meneja wa TBA Mkoa wa Geita Mhandisi Gladys Jefta kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi unakwenda vizuri lakini pia niipongeze TBA kwa kuendelea kutekeleza miradi mingine katika kiwango cha juu,” alisema Ummy.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Luhumbi alimshukuru Rais. Dk John Magufuli kwa kuwapelekea mradi huo wa hospitali ambao utasaidia kuokoa maisha ya wanawake wengi wakati wa kujifungua pamoja na wagonjwa wengine watakaofika katika hospitali hiyo ya Rufaa kupata huduma.

Meneja wa TBA Mkoa wa Geita, Mhandisi Gladys Jefta amemshukuru Waziri wa Afya kwa kutembelea mradi huo wa Afya ambao unatekelezwa na TBA kwa mfumo wa buni – jenga (Design & Build).

“Pia nimefarijika sana kuona Waziri ametambua kazi inayofanywa na TBA kuwa ni yenye ubora na kwamba nitayafanyia kazi yale yote ambayo Waziri ameagiza tuyafanye lakini pia nampongeza Rais wetu  Dk John Magufuli kwa kuwekeza kwenye Sekta ya Afya,” alisema Mhandisi Gladys.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles