30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa aeleza sababu mabalozi kurudishwa nchini

Faraja Masinde -Dar es salaam

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametaja sababu ya baadhi ya mabalozi kurejeshwa nyumbani muda mchache baadaya uteuzi kuwa ni kutokana na kushindwa kufanya chochote katika kutangaza utalii wa nchi.

Majaliwa aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye hafla iliyoandaliwa na viongozi wa dini nchini ya kumpongeza na kumuombea dua, Rais Dk. John Magufuli kwa kuleta mageuzi kwenye sekta mbalimbali.

Alisema serikali imetangaza mpango mahususi kwa ajili ya utalii wa nchi kwa mabalozi wote wa Tanzania ambapo imekuwa ni moja ya jukumu la mabalozi hao.

“Changamoto tuliyonayo ni baadhi ya mataifa kutangaza vitu vyetu kuwa ni mali yao, lakini tumeshaandaa mpango kupitia mabalozi wote wa Tanzania walioko kwenye nchi mbalimbali, moja kati ya jukumu lao ni kutangaza utalii wa nchi.

“Rais (Dk. Magufuli) hajaenda Ulaya wala hana mpango, mimi nimeenda kufuatia kama wanafanya na wanatangaza na tumewapa masharti yakuleta taarifa kila baada ya miezi mitatu, kuwa wamefikia hatua gani, tunalinganisha taarifa ya awali na hii mpya haina chochote tunakurudisha nyumbani tunapeleka mtu ambaye atatengeneza  chochote.

“Hatuwezi kukutambua kuwa wewe ni balozi wetu ukatutangaze alafu unakaa miezi mitatu au sita hun ajambo la kufanya si bora urudi, wote wanajua na tunasimamia, kwahiyo mkisikia mtu ameenda na kurudi msishangae,” alisema Majaliwa.

Alisema kwenye suala la utalii mabalozi hao wanaendelea kutangaza mliama wetu Kilimanjaro kwamba uko Tanzania na ukitaka kuupanda lazima uje nchini.

Alisema kwenye utalii Tanzania inaenda vizuri kwa kutumia mabalozi wetu na wengi wanafanyakazi nzuri.

“Nchi kama China, Israel, Ujerumani, Uingereza nchi nyingine zilikuwa na maneno maneno lakini wanatuletea na sisi tunajua namna ya kukaa nao, sisi ni wazuri kukaa na watu kwa hiyo utalii tunaufanyia kazi,” alisema Majaliwa.

Uchaguzi Mkuu

Aidha, waziri mkuu aliwakumbusha viongozi wanaopata futrsa zakuzungumza mbele za watu kuacha maneno yenye kuondoa utu, dharau na hata  kuvunjiana heshima hususan kuelekea kipindi cha kampeni.

Alisema serikali haitasita kumchukulia hatua yeyote atakayefanya kampeni za ubaguzi na kwamba itafutralia kila kota kuona.

Aidha, kuhusu sababu ya uchaguzi Mkuu kufanyika Jumatano Oktoba 28 badala ya 25, Majaliwa alisema kuwa waliamua kufanya hivyo kutokana na kutambua mchango wa dini na kuondoa kero iliyokuwa ikijitokeza dakika za mwisho.

“Tumeacha Ijumaa Waislamu mwende Msikitini, tumeacha Jumamosi Wasabato mwende kanisani na tumeacha Jumapili Wakristu mwende kanisani, huru kabisa ni Jumatano hiyo haijafanywa makusudi kwasababu tunatambua kero ya Watanzania,” alisema Waziri Mkuu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles