26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Ummy: Hakuna ushahidi corona kuenezwa kwa njia ya damu

 AVELINE KITOMARY– DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha virusi vya ugonjwa wa corona vinaweza kuambukizwa kwa njia ya damu, hivyo kuwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi kutoa na kuongezewa damu.

Waziri Ummy, pia alisema wizara hiyo kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama, wameweka mikakati mbalimbali ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona kwa watu wanaojitokeza kuchangia damu na watoa huduma.

Akizungumza wakati wa maadhimishio ya siku ya wachangia damu duniani jana, Ummy alisema Tanzania inaungana na mataifa mengine kutambua mchango mkubwa unatolewa na wachangia damu kwa hiari.

“Katika kuadhimisha siku ya watoa damu , Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama tunafanya maadhimisho hayo kwa kuwahamasisha wananchi kupitia vyombo vya habari ili waendelee kuchangia damu maeneo mbalimbali yaliyoandaliwa au kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

“Imebainika hakuna ushahidi wa kisayansi unaobainisha virusi vya corona vinaenea kwa njia ya damu, ikiwemo kuongezewa damu na kuchangia damu hivyo nawahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kuchangia damu ili tuwe na damu ya kutosha.

“Katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona mpango wa damu salama, umeweka mikakati mbalimbali ya kuzuia maabukizi ya virusi vya corona kwa wachangia damu na watumishi katika vituo vya kuchangia damu,niwatoe wasiwasi wananchi wote kujitokeza kwa wingi kuchangia damu kwa kuwa tumeweka mikakati kuhakikisha tunazuia maambukizi ya virusi vya corona,”alisema.

Alisema Licha ya maadhimsho hayo kulenga zaidi kuwashukuru wachangia damu, pia malengo mengine ni kukuza uelewa wa jamii katika kutambua kuwa kuchangia damu ni tendo la huruma ,utu,upendo kwa kuwajali watu wengine wenye uhitaji kuboresha afya zao hususan kinamama wajawazito,watoto wa umri wa chini ya miaka mitano pamoja na watu wengine wanaohitaji.

“Lakini yanalEnga kuhamasisha watu ambao hawajawahi kuchangia damu ili waanze kuchangia damu , pia yanalenga kuongeza idadi ya wachangia damu wa mara kwa mara ili kuhakikisha upatikanaji wa damu salama na ya kutosha katika vituo vya afya.

“Kingine ni kujenga jamii yenye mshikamano na hamasa ya kuchangia damu mara kwa mara ili kuwe na akiba ya kutosha ya damu salama,Kukuza ushirikiano wa kitaifa na kimataifa,”alisema.

Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni “ damu salama inaokoa maisha.

“Kauli mbiu hii ya kampeni ya mwaka huu inaonesha mchango wa kila mchangia damu kuweza kuisaidia kuokoa maisha ya mtu mmoja mmoja ,pia inatupa fursa ya kutathimini mikakati ya kuhakikisha taifa letu linakuwa na damu salama na mazao yatokanayo na damu.

“Maadhimisho ya mwaka huu yamehusisha vituo vya kanda vya damu salama kutoa elimu kwa wanachi juu ya kuchangia damu kwa hiari kupitia vyombo vya habari.

“Vituo vya kanda na timu za halmashauri zimeelekezwa kushiriki kampeni za kuhamasisha na kutoa elimu ya uchangiaji damu kwa wananchi,tutaendelea kutoa elimu kwa watoa huduma juu ya namna sahihi ya kwa kinamama wajawazito ,hii ni wakati wakiwa wajawazito na baada ya kujifungua,”alisema.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano, mpango huo,umefanikiwa kuongeza idadi ya chupa za damu salama kutoka chupa za damu 104,632 zilizokusanywa, kupimwa na kusambazwa mwaka 2015 na kufikia chupa 309,376 zilizokusanywa mwaka 2019.

“ Kuna ongezeko la chupa 204,744 sawa na asilimia 195, ikilinganishwa na chupa za damu zilizokusanywa mwaka 2015 na ndio maana tumeona kwa kiasi kikubwa kupungua malalamiko ya upungufu wa damu salama katika vituo vya afya.

 “Wizara tumeboresha huduma kwa kuwapatia mashine za kisasa za kupimia damu uwekezaji huo umegharimu takribani shilingi milioni 13.

“Kwa kutumia mashine hizo mpango wa taifa wa damu salama unaweza kufanya vipimo 4,000 kwa saa sita kutoka vipimo 1,404 kwa mashine zilizokuwepo awali,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles