30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Baba aliyetaka kuozesha mwanafunzi wa miaka 12 atiwa mbaroni Arusha

 JANETH MUSHI– ARUSHA

JESHI la Polisi mkoani Arusha, limefanikiwa kuzima jaribio la mwanafunzi wa shule ya msingi mwenye umri wa miaka 12,aliyetaka kuozeshwa na wazazi wake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shanna,alisema wanashikilia watu wawili akiwemo baba mzazi wa binti huyo, Saiboka Memriki na mwanaume aliyetaka kumuoa binti ambaye ana umri wa miaka 45.

Alisema siku za hivi karibuni, kumeibuka wimbi la baadhi ya wazazi wenye tamaa ya fedha na mifugo kuozesha watoto wao ambao ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao wako majumbani kutokana na ugonjwa wa corona.

Alisema tukio hilo, lilitokea Kata ya Musa wilayani Arumeru,ambapo kabla hawajafanikisha mpango wa kumuozesha mwanafunzi, polisi kwa kushirikiana na wananchi walitoa taarifa.

“Hivi karibuni kuna wimbi limeibuka la watu hususani wenye tamaa ya mahari katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wako nyumbani kutokana na corona kutumia nafasi hiyo kuozesha wanafunzi,”alisema

“Huko Kata ya Musa wazazi walitaka kumwozesha mtoto wao kwa mwanaume, kabla hawajafanikisha nia yao hiyo ovu, jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kudhibiti tukio na kukamata na baba mzazi na mwanaume aliyetaka kumuoa mwanafunzi huyo.

“Kwa bahati mbaya mchezo huo mchafu unashirikisha wazee wa kimila,baadhi ya viongozi wa serikali ya vitongoji na vijiji na wenye tamaa ya fedha na mifugo.Nasema kwa dhati kamwe hatutakuwa na huruma kwa yoyote ayakayemuozesha mwanafunzi,”

“Na kama kuna yeyote aliyepokea mahari kwa mtoto wake hakika tutampeleka jela na kama kuna yeyote alikula hela ya ushenga kwa kufanikisha zoezi hilo ovu nasema ataitapika,kama wananchi wa kawaida au jirani,ndugu na jamaa alikula chakula katika sherehe hiyo kitamtokea puani,”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles