27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waziri Mkuu Majaliwa awatahadharisha wanaoharibu maeneo ya utalii

Anna Potinus – Dar es salaam

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa tahadhari kwa vinara wanaojihusisha na uharibifu wa maeneo ya utalii, waache kufanya hivyo kwa kuwa hatua za kisheria zitazidi kuchukuliwa dhidi yao.

Pia amewataka watanzania watunze maeneo hayo kwa lengo la kukuza mapato kupitia utalii.

“Ningependa kuwakumbusha kuwa baadhi ya  vinara wanaojihusisha, kuharibu vyanzo, kuua wanyama na kufanya uharibifu wamaeneo ya utalii, adhabu zinaendelea kuchuliwa maana wapo baadhi ya watu wanaharibu maeneo ya kale bila kufahamu maeneo hayo ni Tunu ya nchi yetu, hivyo niwaombewatanzania waendelee kutunza maeneo haya ili yalete tija,” amesema.

Amesema kupitia Chaneli hiyo taifa litanufaika kwa kupata idadi kubwa ya watalii ambayo itatusaidia kuingiza mapato zaidi pia itasaidia kuonyesha watalii wa waliopo nje ya Tanzania vivutio vyetu na kuwavutia kuja nchini.

“Tukiimarisha utalii sekta hii itatoa ajira kwa watanzania zaidi ya milioni 1.5 cha muhimu tujiulize kwanini tunabaki nyuma wakati tuna vivutio vingi zaidi,”  amesema Waziri Mkuu.

Aidha amewataka watayarishaji wa vipindi vya runinga hasa vipindi vya utalii kuhakikisha vinavutia kama vile vinavyooneshwa katika chaneli za kimataifa na kwamba hawana budi kupambana na changamoto zitazojitokeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles