27.8 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

mtandao polisi wanawake Arusha watoa msaada

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

BAADHI ya wajawazito waliojifungua na wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru), wameushukuruMtandao wa Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF NET) kwa kuwapa msaada wakibinadamu.

Mtandao huo kupitia Dawati la Jinsia na Watoto, unatoa huduma kwa wananchi kwa lengo la kuelimisha ikiwamo kusimamia haki na sheria ili vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa jinsia zote usiendelee.

Akizungumza mbele ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhan Ng’anzi ambaye ni mlezi wa mtandao huo, Kaimu Mwenyekiti wa TPF NET, Edith Makweli, alisema askari hao wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu juu ya vitendo vya ukatili.

Alisema kutokana na kutambua umuhimu wa jamii wanayoihudumia walitembelea Hospitali ya Mount Meru, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa jinsia kwa wanawake na watoto.

“TPF NET imekabidhi wagonjwa, wanawake wajawazito na waliojifungua msaada wa vitu mbalimbali ikiwamo sabuni, dawa za meno, khanga, sabuni na baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi kwa hospitali hiyo,” alisema Makweli.

Alisema mbali ya kutoa msaada huo kwa upande wao wataendelea kutoa elimu juu ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji ambapo kwa sasa wameamua kupiga kambi maeneo ya pembezoni mwa mji.

“Tumejipanga kufika vijijini kwa nia ya kuwafuata na kuwapa elimu na kutatua changamoto zinazowakabili na siku za usoni utaona mabadiliko makubwa hasa upungufu wa vitendo vya ukatili na unyanyasaji,” alisema Makweli.

Kwa upande wake, aliyejifungua mtoto njiti, Rehema Mollel, aliushukuru mtandao huo wa askari polisi wa kike kwa kuwakumbuka wanawake na wagonjwa wengine.

Naye RPC Ng’anzi akizungumza kwenye maadhimisho hayo aliipongeza TPF NET kwa kuonyesha sura ya kibinadamu ya kuwatembelea wagonjwa na kuwapa msaada wa kibinadamu.

“Madhumuni ya mtandao huu ni kujenga mshikamano na kuhudumia wananchi leo tunaona mkionyesha kwa vitendo kwa kuwaona wagonjwa, hii ni jambo muhimu kwenu na kwetu,” alisema RPC Ng’anzi na kuongeza:

“Huu ni mfano wa kuigwa imekuwa mara chache sana kusikia kero na malalamiko kutoka kwa askari wa kike mmekuwa waadilifu, niendelee kuwaomba muwe mabalozi wazuri mitaani mnakopita.

Alisema kazi zinazofanywa na TPF NET zimesaidia kwa kiwango kikubwa kutokomeza vitendo vya ukali hivyo akiwa mlezi wao aliwaahidi kuendelea kuwapa ushirikiano.

Aidha, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya akina Mama na Watoto Hindu Mbwego alimuomba RPC Ng’anzi kuangalia namna ya kusaidia dawati la jinsia kupatiwa usafiri.

Katika hatua nyingine Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mount Meru Dk. Shafii Msechu aliushukuru mtandao huo kwa msaada walioutoa.

“Kitendo hiki kimetupa ari ya kukamilika kituo cha watu wanaofanyiwa vitendo vya ukatili, mtu akibakwa au kufanyiwa ukatili wowote akifika hapa anakuta huduma zote kwa wakati mmoja hivyo tutaomba kuwe na askari polisi tutakaye saidiana naye,” alisema Dk. Msechu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,340FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles