Yamoussoukro, Ivory Coast
Waziri Mkuu wa zamani wa Ivory Coast, Guillaume Soro, amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Soro, ambaye pia aliwahi kuwa kiongozi wa waasi, ameshukiwa na rungu hilo baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki kuuchafua Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Katika kesi ya msingi, Soro na wenzake 19 walishutumiwa kuhusika katika vitendo vilivyohatarisha usalama wa nchi hiyo. Huku yeye akiangukiwa na adhabu hiyo, kaka zake wawili na rafiki yake wamehukumiwa vifungo vya miaka 17. Mbali ya vifungo, pia wote wametakiwa kuilipa Serikali faini ya Dola za Marekani milioni 179.