24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU ITALIA AJIUZULU BAADA YA KUKATALIWA KUREKEBISHA KATIBA

WAZIRI Mkuu wa Italia, Matteo Renzi
WAZIRI Mkuu wa Italia, Matteo Renzi

ROME, ITALIA

WAZIRI Mkuu wa Italia, Matteo Renzi, amejiuzulu baada ya kukataliwa mapendekezo ya kuifanyia mabadiliko Katiba ya nchi kupitia kura ya maoni iliyofanyika juzi.

Akihutubia taifa kupitia televisheni baada ya matokeo ya awali kutangazwa, Renzi alisema majukumu ya Serikali yake yamemalizika siku hiyo na kuwa anawajibika kikamilifu kwa kilichotokea.

Matokeo hayo yanaonyesha kambi yake ya kura ya ‘Ndiyo’ iliyopigania mabadiliko hayo imeshindwa kwa kupata kati ya asilimia 42 na 46, huku kambi ya ‘Hapana’ inayoongozwa na Vuguvugu la Nyota Tano – M5S, ambalo linapinga sera za wahamiaji, ikiwa imepata asilimia 59.5 ya kura.

“Leo (juzi) demokrasia ya Italia imezingatia mfumo wa Bunge. Nasikitika inanibidi niondoke bila kujutia chochote, kwa sababu demokrasia na kambi ya ‘Hapana’ imeshinda,” alisema.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, asilimia 70 ya watu wanaoruhusiwa kupiga kura walijitokeza vituoni kupiga kura.

Waziri Mkuu huyo amewapa pole wale wote waliokuwa kambi ya ‘Ndiyo’ na amewapongeza kwa kampeni nzuri waliyoifanya.

Renzi ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Italia kwa miaka miwili na nusu, jana mchana alitarajia kufanya kikao cha mwisho na baraza lake la mawaziri kabla ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwa Rais Sergio Mattarella.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles