28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu Ethiopia ajitosa mzozo wa jeshi, waandamanaji Sudan

Sudan 

WAZIRI Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amewasili mjin Khartoum kujaribu kupatanisha watawala wa kijeshi na makundi ya upinzani.

Viongozi wa makundi yanayopigania uhuru na mabadiliko nayayotaka demokrasia nchini humo, yamekataa mazungumzo zaidi na yametoa wito wa kuvunjwa kwa kikosi cha uingiliaji kati cha wanamgambo – Rapid Support Forces ambacho wanakishuhtumu kua mamia ya watu. 

Wanasema kuwa jeshi lazima likabidhi mamlaka mara moja kwa kwa mamlaka ya kiraia ya mpito.

Kwa miezi kadhaa sasa, baraza la utawala wa mpito la kijeshi nchini Sudan limekuwa na utashi mzuri wa kuwa na ushirikiana na mataifa.

Lakini kutokana na taarifa za mauaji ya waandamaji na kuendelea kwa mateso na vitisho dhidi ya raia, kumezua lawama nyingi dhidi ya utawala wa mpito wa kijeshi.

Muungano wa Afrika tayari umetoa wito wa kufanyika uchunguzi juu ya mauji ya hivi karibuni na imetishia kuwawekea vitisho maofisa binafsi wanaokwamisha mchakato wa kipindi cha mpito kuelekea demokrasia.

Waziri Mkuu wa Ethiopia ambaye alifika Sudan jana, anaangaliwa kama mwana mageuzi na alikwishakutana na baraza la jeshi awali. 

Hata hivyo utatakiwa ushawishi mkubwa katika makubalino na Majenerali ili kuweza kuanzishwa kwa mazungumzo mapya ya uundwaji wa Serikali.

Muungano wa Afrika umetaka uchunguzi kufanywa kuhusu mauaji ambayo yanadaiwa kutekelezwa na vikosi vya usalama.

Waandamanaji Sudan mazungumzo

Waandamanaji nchini Sudan, wamekataa ombi la kufanya mazungumzo lililotolewa na baraza la mpito la kijeshi, badala yake wanataka haki kutendeka baada ya jeshi kuwauwa waandamanaji.

Kamati ya madaktari wa Sudan wanaojihusisha na vuguvugu la maandamano hayo, imesema watu 108 wameuliwa katika uvamizi wa jeshi dhidi ya waandamanji waliokuwa wamekita kambi nje ya makao makuu ya jeshi na miili 40 ilipatikana ndani ya mto huku watu zaidi ya 500 wakiendelea kuuguza majeraha.

Msemaji wa muungano wa wasomi wa Sudan unaoongoza maandamano hayo, Amjad Farid, alisema Wasudan hawako tarayi kwa mazungumzo na baraza la kijeshi linalouwa watu.

Alisema wanataka hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wahusika wa mauaji hayo kabla ya kuanza mazungumzo yoyote ya kisiasa.

Farid aliongeza kwamba wataendelea na maandamano bila ya umwagaji damu na kutotii sheria katika kuukataa uongozi wa baraza la kijeshi.

Siku mbili baada ya uvamizi uliosabaisha mauaji hayo makubwa na kulaaniwa kote ulimwenguni, Naibu Kiongozi wa Baraza la kijeshi, Hamdan Dagalo, alisema wameanzisha uchunguzi na wahusika watafunguliwa mashtaka huku akiwataka waandamanji kushiriki katika kikao na baraza la kijeshi kuujadili mkwamo wa kisiasa.

“Mlango wa mazungumzo uko wazi na sisi kama baraza la jeshi tumetangaza mpango kamili wa amani kwa mavuguvugu yote yaliyo na silaha, tumetangaza mpango kamili wa amani kwa wale wote wanaotaka amani lakini hatutavumilia inapokuja katika usalama wa wananchi,” alisema Hamdan.

Daktari Suleiman Abdul Jabbar, katika Wizara ya Afya kupitia Shirika la Habari la Serikali (SUNA), alikanusha taarifa za waandamanaji zinazosema waliouliwa ni zaidi ya 100, akisema hadi sasa idadi ya waliopoteza  maisha hawapiti watu 46. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles