Na FLORENCE SANAWA -MTWARA
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amemuagiza Mrajisi wa Ushirika, Dk. Titto Haule kuangalia kwa umakini utendaji na ufanisi wa Chama cha Ushirika cha MAMCU na viongozi wote ili kubaini kama wanakidhi makusudio yake au laa.
Amesema ikiwezekana chama hicho kivunjwe ili waanzishe vyama kilele viwili vitakavyoweza kuhudumia wakulima katika maeneo yao ili waweze kuongeza tija.
Agizo hilo alilitoa jana wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Chiungutwa wilayani Masasi katika ziara yake anayoendelea nayo mkoani Mtwara.
Pamoja na hali hiyo amerudia kutoa agizo hilo alipozungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Newala.
Alisema anapata shaka kuhusu uwezo wao wa kuwahudumia wakulima, hivyo ameagiza kuharakishwa kwa utekelezaji wa agizo hilo ili kurahisisha utoaji wa huduma.
“MAMCU inahudumia wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Manispaa ya Mtwara, Halmashauri ya Nanyamba, Nanyumbu na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi,” alisema.
Inaendelea…………….. Kwa maelezo zaidi pata nakala yako ya gaziti la #MTANZANIA