24.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU AWAGEUKIA WATENDAJI WA USHIRIKA

Na FLORENCE SANAWA -MTWARA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amemuagiza Mrajisi wa Ushirika, Dk. Titto Haule kuangalia kwa umakini utendaji na ufanisi wa Chama cha Ushirika cha MAMCU na  viongozi wote ili kubaini kama wanakidhi makusudio yake au laa.

Amesema ikiwezekana chama hicho kivunjwe ili  waanzishe vyama kilele viwili  vitakavyoweza kuhudumia wakulima katika maeneo yao ili waweze kuongeza tija.

Agizo hilo alilitoa jana wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Chiungutwa wilayani Masasi katika ziara yake anayoendelea nayo mkoani Mtwara.

Pamoja na hali hiyo amerudia kutoa agizo hilo alipozungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Newala.

Alisema anapata shaka kuhusu uwezo wao wa kuwahudumia wakulima, hivyo ameagiza kuharakishwa kwa utekelezaji wa agizo hilo ili kurahisisha utoaji wa huduma.

“MAMCU inahudumia wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Manispaa ya Mtwara, Halmashauri ya Nanyamba, Nanyumbu na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi,” alisema.

Inaendelea…………….. Kwa maelezo zaidi pata nakala yako ya gaziti la #MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,264FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles