27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waziri Mkuu aagiza uchunguzi milioni 700 za ukarabati wa hospitali Nachingwea

Mwandishi Wetu, Lindi



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi kuunda timu ya wataalamu kufuatilia Sh milioni 700 zilizotolewa na Serikali kukarabati Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea ambazo hadi sasa hazijatumika.

Aidha, ameitaka timu hiyo pia kukagua matumizi ya Sh milioni 400 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi Kituo cha Afya cha Kata ya Kilimarondo ambazo zimeisha kabla ujenzi haujakamilika.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo jana Jumamosi, Novemba 17, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kilimarondo, Nachingwea mkoani Lindi, baada ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha afya.

“Serikali haitaki mzaha na fedha za umma, hivyo Mkuu wa Mkoa unda timu ya wataalamu kutoka mkoani waje Nachingwea kufuatilia ni kwa nini fedha zimetolewa tangu Julai ili kukarabati hospitali ya wilaya ziwe hazijatumika hadi leo. Pia tujue kama kweli bado zipo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles