28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waziri Biteko aagiza kuanzishwa soko la madini Bunda

Na Mwandishi Wetu, Bunda

Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Afisa Madini Mkazi na Katibu Tawala wa Mkoa kuhakikisha wanafungua Soko la Madini wilayani Bunda Mkoa wa Mara ili kuwarahisishia wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kupata huduma hiyo karibu.

Dk. Biteko ametoa agizo hilo leo Jumanne Desemba 28, 2021 wakati akizungumza na wachimbaji katika eneo la Kinyambwiga lililopo Kata ya Guta wilayani Bunda mkoani Mara.

Wachimbaji wakimsikiliza Waziri wa Madini, Dk. Dotto Biteko.

Amesema haiwezekeni mchimbaji ana dhahabu yake mfukoni anaenda hadi Musoma kutafuta soko nakwamba ni lazima soko la madini lianzishwe Bunda ili watu wafanye biashara ya madini kwa urahisi.

“Natoa agizo kwa Mkuu wa Wilaya, Afisa Madini na Katibu Tawala wa Mkoa ambaye kwa mujibu wa kanuni ya uanzishwaji wa masoko ya madini ndiye mwenye kutafuta eneo sahihi ya kuweka soko la madini,” ameongeza Dk. Biteko.

Ameongeza kuwa, bado kuna umbali mkubwa hivyo kutoka eneo la machimbo mpaka Bunda na kuwataka kianzishwe kituo kidogo cha kununua madini katika eneo la Kinyambwiga.

Amesema, eneo litaandaliwa kwa wafanyabiashara wa madini (Brokers) ili biashara yote ifanyike katika eneo hilo la wachimbaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles