24.3 C
Dar es Salaam
Monday, September 16, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Bashe akikabidhi Mradi wa Umwagiliaji wa Bonde la Luiche

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (Mb) leo Julai 21,2024 ameshiriki katika hafla ya kukabidhi mradi wa umwagiliaji wa Bonde la Luiche, mkoani Kigoma kwa mkandarasi M/S CRJE (East Africa) LIMITED ya Dar es Salaam.

Mradi huu, unaogharimu Sh Bilioni 65.16, unahusisha ujenzi wa bwawa, mfereji mkuu wa maji, uchimbaji wa mitaro, barabara za mashambani, nyumba za watumishi, ofisi za wahandisi, ghala, na mashine ya kukoboa mpunga.

Akitoa salamu za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mkurugenzi Mkuu, Raymond Mndolwa alisema mradi huu utakaogharimu Sh Bilioni 65.16, utahusisha ujenzi wa bwawa, mfereji mkuu wa maji, mitaro ya mashamba, barabara za mashambani, nyumba za watumishi, ofisi za wahandisi, ghala, na mashine ya kukoboa mpunga.

“Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imejipanga kuhakikisha wananchi wa Bonde la Luiche wananufaika na mradi huu. Tunampongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kukuza kilimo cha umwagiliaji,” alisema Mndolwa.

Waziri Bashe alisema mradi huu, utakaozalisha eneo la hekta 3,000, utanufaisha wakulima zaidi ya 9000 katika kata za Kagera, Simba, na Mungonya, mkoani Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. CGF (mstaafu) Thobius E. M. Andengenye alieleza kuwa zaidi ya Shilingi Bilioni 60 zilizotengwa kwa mradi huu ni hatua muhimu kwa wananchi wa Luiche na Kigoma kwa ujumla.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Ng’enda Kirumbe, alitoa shukrani kwa Wizara ya Kilimo kwa mradi huu ambao umekuwa ukizungumziwa tangu Uhuru. “Mradi huu unathibitisha maendeleo na kuongeza mzunguko wa fedha kupitia kilimo cha umwagiliaji,” alisema Kirumbe.

Mkoa wa Kigoma una zaidi ya hekta 120,000 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, lakini kwa sasa, ni hekta 9,070 pekee zinazomwagiliwa kupitia mabonde na skimu 59.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles