25.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

Wawili wakamatwa na Polisi tuhuma za mauaji ya mtoto wa miezi minne Bukoba

Renatha Kipaka, BUKOBA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikiria watuhumiwa wawili wa mauaji ya mtoto wa miezi minne yaliyotokea Novemba 9,2024 ,katika kijiji cha Itahwa Kata ya Kalabagaine wilayani Bukoba mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi mkoani hapo Blasius Chatanda amesema,wakiwa katika maandalizi ya kutenda tukio hilo mmoja wa watuhumiwa hao aitwaye Maria Christian( 62) mkazi kijiji cha Nkindo ambaye ni jirani alikuwa akitwanga dawa ya kienyeji ambayo katika uchunguzi wa tukio hilo iligundulika mtoto huyo alikiwa amepakwa dawa usoni .

“Mtoto huyo alikutwa amepakwa dawa ya kienyeji katika paji la uso hali inayotoa picha kwamba kunauwezekano mkubwa suala hilo lilihusiana na imani za kishirikina,” amesema Chatanda.

Amesema mtuhumiwa wa pili Selina Prospa ( 45) mkazi wa kijiji cha Nkindo ambaye ni mama wa kambo wa baba wa mtoto huyo alimtuma dukani mtoto wake ili atoe nafasi ya wawili hao kufanya uharibifu waliokuwa wameupanga.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mjini Bukoba

Aidha amesema wakati wanafanya mauaji hayo mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa ametoka kwenda dukani na kumwacha mwanae akiwa amelala ndani ya nyumba.

Ameongeza kuwa mara baada ya kurudi nyumbani mama huyo aliingia ndani ya nyumba na alipomwangalia mwanaye alibaini kuwa amejeruhiwa kwa kukatwa katika kikanja cha mkono wake.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi mkoani hapo linamshikiria Merchad Tiba (68)mkazi wa kijiji cha Burimo Kata Kibanga wilayani Muleba mkoani Kagera kwa tuhuma za kujaribu kuchoma moto ofisi ya mtendaji wa kijiji.

Kamanda alibainisha kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 9, 2024 na kwamba kabla ya kijaribu kuchoma aliweka majani makavu na kipande cha godoro ingawa moto haukufanikiwa kuwaka ili kuunguza jengo.

Kamanda amesema kwa taarifa ambazo jeshi hilo lilizipata, mtuhumiwa ni kwamba alipanga kutekeleza tukio hilo ili kuteketeza nyaraka zote zilizokuwemo katika ofisi hiyo kwa maslahi binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles