UONGOZI wa Serikali mpya ya kijeshi ya Guinea umeingia nyumbani kwa waziri wa viwanda wa zamani wa nchi hiyo, Tibou Kamara, na kisha kumshikilia kwa mahojiano, kabla ya kumwachia saa chache baadaye.
Baada ya kuingia nyumbani kwa Kamara, wanajeshi waliokuwa kwenye sare zao walimpokonya simu na kuondoka naye kusikojulikana. Chanzo kinaeleza kwamba sababu kubwa ya kiongozi huyo kuwekwa kitimoto ni kitendo chake cha kuvunja ahadi kuwa angekaa kimya juu ya utawala wa kijeshi unaoendelea Guinea.
Inafahamika kuwa Kamara pia alikuwa mshahuri wa rais aliyeondoshwa na jeshi madarakani, Alpha Conde