26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mastaa wanaoitangaza Kenya huko majuu

KAMA zilivyo nchi nyingi za Afrika, Kenya nayo ina idadi kubwa ya mashabiki wa mchezo wa soka.

Licha ya timu yake ya taifa ‘Harambee Stars’ kutokuwa tishio, Kenya ina utitiri wa wachezaji wanaokipiga Marekani na barani Ulaya.

Victor Wanyama – Montreal Impact Kwa sasa, kiungo huyo ndiye mchezaji mwenye mafanikio zaidi kwa Kenya. Si kwa klabu kubwa alizocheza, bali pia kwa mkwanja aliokusanya kwenye soka la kulipwa. Achana na Inter Milan, Wanyama amecheza England alikowahi kuzitumikia kwa miaka saba klabu za Southampton na Tottenham. Anaitumikia Montreal Impact ya Canada inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani.

Michael Olunga – Al Duhail Mshambuliaji huyo alijiunga na klabu hiyo ya Qatari mwaka huu. Ameifungia Harambee Stars jumla ya mabao 19 katika mechi 44. Kwa Qatar, analipwa KSh milioni 16 (zaidi ya Sh mil. 330 za Tanzania) kwa mwezi.

Michael Olunga

Joseph Okumu – Gent Ni beki wa kati mwenye umri wa miaka 24 anayekipiga Gent ya Ligi Kuu ya Ubelgiji. Kwa miaka mitatu iliyopita, amecheza soka Amerika na Ulaya. Alitua Gent mwaka huu, usajili wake ukigharimu Ksh milioni 439 (zaidi ya Sh bil. 9 za Tanzania). Okumu amecheza mechi tisa akiwa na uzi wa Harambee Stars.

Eric Otieno – AIK Fotboll Mlinzi wa kushoto huyo mwenye umri wa miaka 24 amecheza mechi 26 akiwa na Harambee Stars na kwa sasa anakipiga AIK Fotboll ya Ligi Kuu ya Sweden aliyojiunga nayo mwaka jana akitokea Vasalund ya nchi humo. Kutokana na kiwango kizuri alichonacho, saini yake imeanza kuzivutia klabu kadhaa za Ligi kubwa tano za Ulaya na mkataba wake na AIK Fotboll utakwisha mwaka 2024.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles