25.4 C
Dar es Salaam
Thursday, January 9, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waziri ataka maghorofa Magomeni kota ukamilike Juni 30

Tunu Nassor -Dar Es Salaam

FAMILIA zaidi ya 600 zilizokuwa zikiishi katika Kota za Magomeni zinatarajiwa kurejea katika eneo hilo Juni 30, mwaka huu baada ya Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) kukamilisha ujenzi wa majengo hayo.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo na kuangalia maendeleo ya ujenzi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe, amewaagiza TBA kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa mradi huo ifikapo Juni 30.

Kamwelwe alisema Serikali inaridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo lakini anautaka uongozi wa TBA kufanya juhudi ili mradi huo ukamilike na familia hizo zianze kuingia.

“Ifikapo mwisho wa mwezi Juni tunataka kazi iwe imeshakamilika na zoezi la kuhamishia watu zaidi ya 600 katika majengo haya lianze rasmi, imani yangu kazi ujenzi huu utakwenda vizuri kwani tunataka  mwishoni mwa mwezi Mei baadhi ya familia tuanze  kuziingiza katika majengo haya,” alisema

Alisema majengo hayo kama hayatakamilika kwa wakati na muda aliousema basi Mtendaji Mkuu wa TBA, Daud Kondoro atapaswa kujiuzuru katika nafasi yake.

Waziri Kamwelwe, alisema miundombinu ya maji na umeme inaendelea kuwekwa katika majengo hayo ili Juni 30 mwaka huu viwe vimekamilika na watu wahamie.

Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TBA, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Umiliki TBA, Said Mndeme alisema  watatekeleza maagizo ya Serikali kama yalivyotolewa hivyo itakavyofikia Juni kila kitu kitakuwa tayari.

“Tumepokea maelekezo ya waziri ya kuhakikisha tunakamilisha mradi huu kwa wakati, tumejipanga vema na kiuhalisia zoezi ili litakamilika Juni 30 mwaka huu, katika majengo haya tupo katika hatua ya mwisho,” alisema.

Mndeme aliwahakikishia wakazi wa eneo hilo kuwa wataingia katika majengo hayo kwa muda uliowekwa na Serikali.

Ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi kutekelezwa mwaka 2017 baada ya kuzinduliwa  na Rais Magufuli ambapo ulitarajiwa kukamilika mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles