25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waziri aliyetoka jela ashikiliwa tena Sudan

KHARTOUM, Sudan

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan wakati wa utawala wa Rais Omar al-Bashir, Ibrahim Ghandour, ameshikiliwa na vyombo vya usalama kwa mara nyingine, zikiwa ni saa chache tu tangu alipotoka gerezani.

Ghandour mwenye umri wa miaka 68, sambamba na vigogo wengine wawili waliokuwa karibu na al-Bashir, waliachiwa huru baada ya jeshi kupindua Serikali hivi karibuni, hatua iliyokosolewa vikali.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kile kilichoelezwa na familia katika mahojiano yake na Reuters, leo mwanasiasa huyo amerejeshwa kwenye mikono ya vyombo vya usalama.

Hayo yanatokea wakati bado Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inaendelea ‘kumtamani’ al-Bashir kwa kile inachoamini utawala wake ulihusika katika vifo vya watu 300,000 katika machafuko mjini Darfur.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles