25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI AJIUZULU KUPINGA UFISADI ZAMBIA

LUSAKA, ZAMBIA


WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Zambia, Harry Kalaba, amejiuzulu juzi jioni akipinga kushamiri kwa vitendo vya rushwa serikalini.

Katika ujumbe wake alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook, Kalaba alisema alishakabidhi barua yake ya kujiuzulu wadhifa huo alioushikiria kwa miaka minne.

“Hatuwezi kuendelea kuendesha masuala ya kitaifa wakati ufisadi umetawala miongoni mwa wale waliotakiwa kuwa mstari wa mbele kutatua tatizo hilo,” alisema.

“Inaonekana kwamba Wazambia masikini si sababu ya uwapo wetu madarakani. Upendeleo na uwekaji mbele fedha umechukua nafasi kubwa katika maamuzi mengi yanayofanywa leo hii,” aliongeza.

Siku moja kabla ya uamuzi huo, Kalaba, katika ujumbe alioutuma katika mtandao wa jamii alilaani rushwa na utawala duni, hatua iliyowakasirisha baadhi ya wanachama wa chama tawala waliomtaka ajiuzulu.

Kalaba aliteuliwa kwa mara ya kwanza kuingia katika Baraza la Mawaziri mwaka 2014 na marehemu Michael Sata na kuendelea na wadhifa wake chiniya Rais Edgar Lungu.

Amekuwa waziri wa tatu kuondoka madarakani baada ya wiki iliyopita Rais Lungu kumtimua Waziri wake wa Mipango na Maendeleo ya Taifa Lucky Mulusa. Aidha Novemba mwaka jana, Rais alimfukuza Waziri wa Habari Chisimba Kambwili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles