Mary Mwita, Hai
Wazee wilayani Hai wamedai kunyanyaswa na wake zao na wakati mwingine kupigwa hali inayochangia kuharakisha vifo vyao kabla ya wakati.
Aidha, wamedai licha ya unyanyasaji huo, hawana mahali pa kujitetea kwa kuwa wao ni wanaume.
Baadhi ya wazee hao kwa nyakati tofauti wamedai idadi kubwa ya wazee wanakufa katika karne hii kutokana na unyanyasaji kutoka kwa wake zao ikiwa ni pamoja na kunyimwa chakula na kusisitiza kuwa hali hiyo isipokemewa itaangamiza wazee wengi.
“Mimi niseme kuwa wazee wanapata shida sana na kutokana na aibu ya kuwa ni wanaume hawatoki nje kupiga kelele hali inayozidisha ukatili jamani wasaidie wazee hawa.
“Wazee Rundugai wangekuwa hawatunzwi na Dorcas Aid Tanzania, wangekuwa wamekufa kwa kuwa wamepewa kisogo na wake na watoto wao,” amesema Mzee Evarest Mvungi ambaye ni Mwanakamati wa Mradi wa Wazee Runduga, Wilaya ya Hai