28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

ALI KIBA AFIKISHWA MAHAKAMANI

NA KULWA MZEE -DAR ES SALAAM


SIKU mbili kabla ya msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba kufunga ndoa katika Mji wa Mombasa, mfanyabiashara wa mitumba aliyezaa naye, Hadija Hassan, alikimbilia mahakamani kudai matunzo.

Hadija alifungua kesi katika Maha089kama ya Watoto iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Aprili 17, mwaka huu, ikiwa ni siku mbili kabla ya Kiba kufunga ndoa na Amina Khaleef, Aprili 19, mwaka huu.

Akieleza katika hati yake ya madai, Hadija anadai ni mkazi wa Magomeni na anafanya biashara ya mitumba na mdaiwa ni mwanamuziki.

Anadai alizaa na Ali Kiba mtoto wa kike Januari 2013, katika Hospitali ya Micco, Dar es Salaam.

Katika madai yake, anadai kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, mdaiwa anatakiwa kumhudumia mtoto huyo kwa mahitaji yote ikiwamo chakula, nguo, elimu na matibabu.

“Kutokana na sheria ya watoto ya mwaka 2009, mdaiwa anatakiwa kutoa huduma kila mwezi, chakula Sh 150,000, matunda Sh 50,000, chakula cha ziada Sh 50,000, michezo na burudani za watoto Sh 100,000, nguo Sh 60,000 na matibabu Sh 50,000 ambapo jumla ni Sh 460,000.

“Mdaiwa anatakiwa kulipa ada ya shule kwa muhula Sh 950,000 aliacha kutoa matunzo kwa mtoto tangu Januari 2018, hivyo naiomba Mahakama imwamuru mdaiwa kutoa matunzo ya Sh 460,000 kila mwezi na ada,” aliomba mdai katika madai yake.

Hadija anaomba malipo ya kwanza yatolewe mapema baada ya hukumu, anaiomba mahakama imwamuru kumsomesha mtoto, kumnunulia nguo na matibabu ikiwamo kumtafutia bima ya afya.

“Naiomba mahakama imwamuru Kiba kulipa gharama za matunzo Sh 460,000 kuanzia Februari 2017 mpaka siku itakapotolewa hukumu na gharama za kesi.

“Naomba mahakama itoe amri nyingine yoyote inayoona inafaa kwa manufaa ya mtoto,” alidai.

Kesi hiyo imefunguliwa kwa msaada wa Kituo cha Msaada wa Kisheria, WLAC.

Ali Kiba alifunga ndoa Aprili 19, mwaka huu, mjini Mombasa na kufuatiwa na hafla kubwa iliyofanyika Aprili 29, mwaka huu, katika ukumbi wa Serena Hotel, jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles