27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wazazi wanaoua watoto wakapimwe akili

Na AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM

TUMESHUHUDIA matukio mengi ya wazazi kuua watoto wao kwa makosa ambayo wangeweza kuwasema na kuwakanya wasirudie kuyatenda.

Ni jambo la kushangaza kuona mama au baba anadiriki kumuu amwanawe wa kumzaa eti labda kwa sababu ameiba fedha au amedokoa chakula.

Matukio kama haya ni ya kufikirisha, kuna uwezekano mkubwa wazazi wa aina hii huwa aidha wamepungukiwa akili au wamepumbazwa akili. Maana hili si jambo la kawaida hata kidogo.

Ukiacha hao wanaoua watoto wao kwa makosa ya hapa na pale,pia wapo ambao wanaua wale ambao hata hawajaonja mapenzi ya wazazi wao hapa duniani. Unaweza kujiuliza wako sawa kiakili?

Tukio kama hili lilitokea hivi juzi tu, ambapo mkazi wa Mburahati NHC, Angelina Joseph (23), alipandishwa kizimbani katika Mahakama yaWilaya ya Kinondoni kwa shtaka la kumuua mtoto wake.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Frank Moshi, Mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Ramadhan Mkimbo, alidai Novemba 5, mwaka huu, eneo la Mburahati NHC Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, mshtakiwa kwa makusudi alisababisha kifo cha mtoto wake wa siku mbili.

Hata hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu tuhuma hizo kutokana na mahakama kutokuwa na uwezo wa kuisikiliza.

Kuna wazazi wengi wa aina hii, ambao hudiriki kuua watoto wao waliowabeba tumboni miezi tisa kwa madai ya kutomudu gharama za malezi,haya binafsi nayaita ni mawazo finyu.

Haiwezekani ubebe mimba miezi tisa, Mungu akakusaidia ukajifungua salama na baada ya hapo uue mtoto eti kwa sababu maisha ni magumu hautaweza kumlea.

Siku zote mtoto anapozaliwa huwa ni wa jumuiya na si mzazi pekee, haiwezekani akashindwa kuishi kwa kukosa chakula au huduma muhimu.

Wapo wasamaria wema ambao wanaweza kujitokeza na kusaidia malezi pindi inapotokea mzazi amekwama.

Kama hiyo haitoshi, mtoto kuanzia siku moja hadi miezi sita huwa anaishi kwa maziwa ya mama tu, sasa kama mzazi umeweza kubeba mimba hadi ukajifungua maana yake hata kama mlo wako ni wa shida lakini umeweza kumudu hali hiyo, hivyo hata mtoto angeweza kuishi kwa sababu anachokula mama ndichoatakachokula mtoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles