29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi wa Kiislamu watakiwa kusaka mwarobaini wa watoto wa kike kukosa elimu

Na Safina Sarwat, Moshi

Mfanyabiashara maarufu Ibrahimu Shayo, amezishauri taasisi za elimu za Kiislamu pamoja na wazazi nchini, kutafuta mwarobaini wa tatizo la watoto wa kike wa dini hiyo kukosa elimu kutokana na mitizamo hasi ya jamii.

Shayo ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya usafirishaji ya Ibra Line, ametoa ushauri huo juzi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la Al -AZHAR Islamic center iliyopo Kata ya Njoro, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

“Hili jambo linalohusu ukandamizaji wa haki za watoto wa kike, hazipaswi kupewa nafasi. Tumeona mara kadhaa, kikwazo kikubwa kwa watoto wa kike wa dini za kiisalam nchini ni kupata elimu kuondokana na hali ya utegenezi,” amesema Shayo.

Amesema kuwa watoto wakipata elimu tutakuwa tumewasaidia vijana hao kujitegemea na kuondokana na dhana ya utegenezi na kuongeza kipato kwani wakipata elimu wataweza kujiajiri wenyewe.

“Tusaidiane kuhakikisha tuna saidia jamii hasa hao watoto wetu wanapata elimu ya dini pamoja na elimu dunia vyote hivyo tukiweza kuwapatia tunazalisha taifa yenye maadili na uadilifu,”amesema Shayo.

Mbali na uwekaji wa jiwe la msingi la jengo hilo ameongoza harambee kwa ajili ujenzi huo jengo ghorofa mbili ambapo jumla fedha zaidi milion saba zilikusanywa.

Awali, akisoma risala mweka hazina wa kamati ya ujenzi, Abubakar Msangi amesema jengo hilo linahitaji zaidi ya Sh million 400, nakwamba ujenzi huo uko katika hatua za awali.

Kwa upande wake katibu wa ujenzi, Sheikh Issa Juma amewaasa wananchi kuendelea kudumisha amani na upendo na kushirikiana katika shughuli za kujenga nyumba za ibada ili kujenga taifa bora lenye mshikamano na uzalendo.

“Tuishi maisha matakatifu tulinde amani yetu ili tusije tukajutia badae, tumwombee sana Rais Samia Suluhu pamoja na viongozi wengine kwani jukumu letu sisi viongozi wa dini,”amesema Juma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles