25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Tumaini jipya kwa wakazi wa Kivule baada ya DAWASA kufufua mradi wa maji JICA

Na Fredy Mshiu, DAWASA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imefufua mradi wa maji KIVULE JICA ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma ya majisafi kwa wakazi walio nje ya mtandao rasmi wa Mamlaka.

Hili limethibitika kwa DAWASA kukamilisha kazi zilizolenga kuboresha mradi huo wa Kivule JICA wenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya wakazi 3,600 wa Kivule.

Akiongelea utekelezaji wa mradi huo Mkurugenzi wa Mawasiliano na jamii wa DAWASA, Neli Msuya, amesema mradi huo ulioacha kufanya kazi mwaka 2019 umefufuliwa baada ya kuona uhitaji na ongezeko kubwa la watu katika eneo hilo.

“Mradi huu umehusisha unusual na ufungaji wa pampu mpya na za kisasa za maji, uchimbaji na ulazaji wa bomba zenye ukubwa mbalimbali kwa umbali wa kilomita 4, lakini pia marekebisho katika mfumo wa umeme,” amesema Neli.

Mbali na hayo ukubwa wa visima vinavyopatikana eneo hili vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita 12,000 na kingine lita 10,000 kwa saa ni sababu nyingine inayopelekea DAWASA kufufua mradi huu wa maji Kivule JICA. Kwa ujumla visima hivyo vina uwezo wa kuzalisha lita 290,000 kwa siku.

Nae Afisa Mtendaji wa mtaa wa Kerezange kata ya Kivule, Isdora Karanga amesema wananchi wameupokea mradi huo Kwa furaha kubwa.

“Tumepokea mradi huu uliofufuliwa na DAWASA kwa furaha kubwa, kwani tulikuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji tangu mwaka 2019 mradi ulipoacha kufanya Kazi huku wananchi wakitumia maji ya visima vya watu binafsi ambayo hayatoshelezi mahitaji yao na gharama zao ni kubwa,” amesema Isdora.

DAWASA inaendelea kuwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupata maunganisho ya maji huku wakihudumiwa kwa ukaribu na Mkoa wa kihuduma Temeke.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles