24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Ukosefu wa chakula shuleni kwatajwa kushusha ufaulu

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Ukosefu wa chakula cha mchana kwa wanafunzi katika baadhi ya shuleni mkoani Kilimanjaro, kumetajwa kuwa moja ya sababu inayosababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu.

Katibu wa Chama cha Walimu nchini (CWT) Mkoa wa Kilimanjaro, Daudi Mafwili ameyasema hayo leo Alhamisi Juanuari 6, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake mjini moshi ambapo amesema kuwa matokeo mabaya yanachingiwa changamoto ya watoto kutopata chakula cha mchana mashuleni.

Amesema kuwa shule ambazo zinafanya vibaya katika mkoa wa Kilimanajaro ukizifuatilia unakuta ni zile ambazo zinachangamoto ya chakula kwa wanafunzi hivyo huwapelekea kushindwa kuhudhuria vipindi vya masomo ipasavyo.

“Kila mtoto  anafundishika endapo atapatiwa chakula cha mchana nakuboreshewa mazingira hivyo sisi kama chama tunaishauri serikali kusimamia vema hili suala shule zote watoto wapate chakula mashuleni,”amesema Mafwili.

Amesema suala la chakula lisipozingatiwa wasitegemee matokeo mazuri na kwamba walimu wasilaumiwe kwa lolote kwani hata wakifundisha mwanafunzi hataweza kuelewa chochote wakati wa njaa.

“Tumejipanga kupeleka ushauri wetu kwa serikali kutekeleza majukumu yake ya kuboresha mazingira ya utoaji elimu na kuhakikisha watoto wote wapata chakula cha mchana,”amesema.

Katika hatua nyingine, ameishauri Halmashauri kutoa motisha kwa walimu wote bila kuwabagua na kusimamia stahiki za walimu.

Diwani kata ya kileo Wilaya ya Mwanga, Kuria Msuya amesema ipo haja ya halmashauri kwa kushirikiana na baraza la madiwani kuweka mikakati ya kuwadhibiti wazazi wanaokataa kulipa fedha za chakula mashuleni ili kuhakikisha wanafunzi wote wanakula chakula cha mchana wawapo shuleni. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles