26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi Ilala wahamasisha ujenzi wa chama kwa bonanza kali

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Bonanza la michezo lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala limefana na kuleta ushindani mkubwa kwa timu shiriki kwenye michezo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa bonanza hilo lililofanyika viwanja vya Stakishari Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala, Idd Mvano, ameagiza matawi na kata za jumuiya hiyo kuandaa mabonanza kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika ujenzi wa chama hicho.

“Tunawashukuru wanachama na wapenzi waliojitokeza tumepata mwitikio mkubwa na tumeona tuendeleze uhamasishaji kwa kuwa na mabonaza kama hili hadi ngazi ya chini yaani kwenye kata na matawi,” amesema Mvano.

Mgeni rasmi katika bonaza hilo Suleiman Juma Kimea ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Wazazi Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, amesema michezo ni afya na ni ajira kwani kupitia bonaza kama hilo wanapata vipaji vipya.

“Kupitia mabonanza tunapata vipaji vya wanamichezo mbalimbali na ni moja katika mambo yetu ya jumuiya ya wazazi, elimu malezi na mazingira. Vijana wanataka kuendelezwa..nawapongeza kwa kazi nzuri mliyofanya,” amesema Kimea.

Akizungumzia mikakati ya baadaye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mohamed Msofe, amesema wanatarajia kuandaa bonaza lingine litakalokuwa na kaulimbiu ya ‘Wazazi Ilala na Uchumi’ sambamba na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa jamii ili wanapochukua mikopo wajue jinsi ya kuitumia na kupata mafanikio.

Amesema pia mkakati mwingune ni wa kujenga nyumba ya katibu na kwamba tayari kiwanja kimepatikana.

“Tuko vizuri wanachama wana ushirikiano mkubwa tunaendelea kufanya kazi kukisaidia chama. Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayofanya kwa sababu kila mtu anaona hasa alivyopambana katika suala la Uviko…tunaendelea kumuunga mkono kuhakikisha kila mmoja anapata chanjo,” amesema Msofe.

Awali Mwenyekiti wa Bonaza hilo Shamsudin Ally Ahmed, amesema lilishirikisha mpira wa miguu kwa wanawake na wanaume, kuvuta kamba, kufukuza kuku, elimu ya Uviko na kuchanja, kuchangia damu, kutoa elimu ya ujasiriamali na ushauri nasaha kwa watumiaji wa dawa za kulevya.

Katika bonanza hilo mshindi wa kwanza kwa mpira wa miguu alizawadiwa mbuzi wakati mshindi wa pili alizawadiwa jezi na mipira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles