25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wawili kortini kwa hasara ya mil 997/-

Na PATRICIA KIMELEMETA -Dar es Salaam


ALIYEKUWA Mkuu wa Ununuzi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Mohammed Ally, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mawili ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya Sh milioni 977.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa mwingine ni Mkaguzi Mkuu wa Ubora wa Bidhaa za Ngozi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Peter Tarimo.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Augustina Mbando, wawakili wa Serikali, Aneth Mavika alidai washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Julai 16 na 30, 2013.

Mavika alidai kwa makusudi wakiwa wajumbe wa uthamini wa zabuni namba AE-054/2013/2014/HQ/9/02 lot namba 01, walitumia madaraka yao vibaya kwa kuipendekeza na kuizawadia Kampuni ya Bajuta International T. Limited ili kushinda zabuni hiyo huku wakijua kuwa haikuwa na sifa.

Alidai katika zabuni hiyo, kampuni hiyo iliwasilisha nyaraka ambayo haikuendana na masharti yaliyoainishwa katika zabuni, jambo ambalo ni kinyume na sheria za ununuzi.

Wakili huyo alidai shtaka jingine linalowakabili washtakiwa hao ni pamoja na kushindwa kutimiza majukumu yao na kuisabaishia NFRA hasara ya Sh milioni 977.

Alidai upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa kutajwa.

Wakili Mavika pia aliiomba mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa wa pili, Edward Mtango ili aweze kuunganishwa katika kesi hiyo.

Hakimu Mbando alikubaliana na ombi hilo na kutoa amri ya kukamatwa kwa mshtakiwa huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles