22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda apigia debe vicoba taasisi za fedha

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


WAZIRI Mkuu mstaafu Mizengo Pinda amezitaka taasisi za kifedha zikiwamo benki kuviamini vikundi vya vicoba katika mikopo ili vipate mitaji ya kujiendesha.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana wakati akifunga maonesho ya Wiki ya Vicoba yaliyoandaliwa na Shirika la Sedit.

“Wito wangu kwa vyombo vya fedha ikiwa ni pamoja na benki, kuvitumia vicoba kwa kuvipa mikopo ili viweze kujiendesha kwa sababu huku kuna watu wengi ambao wapo tayari kufanya shughuli na wamekuwa wakifanya vizuri,” alisema.

Pia alisema wana vicoba wana wajibu wa kuwa chachu ya mapinduzi ya viwanda kwa kuisaidia Serikali kufikia azma hiyo.

“Ninyi wana vicoba mnaweza kuwa chachu ya mapinduzi ya kilimo kama kila mmoja ataweza kutimiza wajibu wake, ila mimi nina imani na ninyi. Niwatie moyo fumbeni masikio tutapita tu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles