31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Wawekezaji waliogeuza viwanda maghala kunyang’anywa Moshi

Safina Sarwatt, Moshi

Mbunge Moshi mjini, Priscu Tarimo ameahidi kwenda kumwomba Rais Dk.John Magufuli kuwanyang’anya wawekezaji waliowekeza kwenye viwanda Moshi na kushindwa kuviendeleza badala yake kugeuza maghala ya kuwekea mizigo na bidhaa huku mengine yakigeuka kuwa magofu.

Akizungumza jana katika mkutano uliofanyika Stend Kuu ya mabasi mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo pamoja na mambo mengine alisikiliza kero za wananchi wa Manisipaa Moshi, Tarimo amesema atahakikisha kwamba atakwenda kumwomba Rais Magufuli kufuta mikataba ya uwekezaji wa viwanda waliopewa wawekezaji hao.

Tarimo amesema kiu kubwa ya wananchi wa Manispaa ya Moshi ni kufufuliwa kwa viwanda ili vijana wapate ajira pamoja nakukuza uchumi wao na wa wilaya ya Moshi kwa ujumla.

“Nitakwenda kumwomba rais pia nikienda bungeni nitapeleka hoja hiyo, viwanda virudi serikalini kwa sababu wawekezaji waliopewa wamekiuka mkataba kwa kushindwa kuviendeleza matokeo yake wamefanya kuwa maghala ya kuhifadhia bidhaa na vingine vimetelekezwa na kuwa magofu,”amesema.

Amesema kuwa kufufuliwa kwa viwanda hivyo ni moja ya ahadi za za rais wakati wa kampeni yake ya kuwaomba kura wananchi wa Manisipaa ya Moshi kwenye mkutano ulifanyika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Akizungumzia changamoto iliyowasilishwa mkutanoni hapo inayohusu huduma bure za afya kwa wazee, amesema lengo la serikali ni kuhakikisha wazee kuanzia umri miaka 65 na kuendelea wale wasiokuwa na uwezo wanapatiwa vitambulisho na kuhudumiwa bure kwenye hospitali zote za serikali.

Changamoto nyingine aliyokutokea tamko ni ile inayohusiana na kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia ambapo amesema hili ni swala la kitaifa hivyo watakwenda kulijadili na wabunge wenzake kwenye vikao vya kibunge .

“Ndugu zangu hilo la kupanda kwa bei ya mafuta ni swala a la kitaifa hivyo nikienda bungeni tutakwenda kulijandili na wenzangu ili kulipatia ufumbuzi wa pamoja, “amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles