Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam
Wizara ya Viwanda na Biashara imewataka wawekezaji wote nchini kuongeza nguvu katika Ujenzi wa Viwanda ili kuongeza thamani katika malighafi zinazotengenezwa nchini hali ambayo itauna kipato cha wakulima.
Hayo yameelezwa leo Julai 14, 2021 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, wakati akizungumza na watengenezaji wa kinywaji cha Kiwingu kutoka Kilimanjaro Biochem ambao wanalengo la kuinua wakulima.
Amesema kuwainua wakulima kwa kutumia malighafi za ndani katika utengenezaji wa Spirit zitokanazo na nafaka za wakulima wa Tanzania.
“Serikali imepambana kuondoa vikwazo vyote kwa wawekezaji ambavyo vilitokana na urasimu wa watendaji wachache wasio na maadili ya Utumishi wa Umma.” amesema Kigahe
Kwa upande wake Meneja Mauzo, Mhandisi Mathias Luhanya, amesema kuwa kampuni yao ya Kilimanjaro imejikita kutengeneza ajira kwa vijana.
“Hadi sasa tuna zaidi ya vijana 200 tumewaajiriwa kwa mwaka kwa ajira za mikataba, lakini tuna mpango wa kuendelea kutoa ajira kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi,” amesema Luhanya