26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

Rais Samia ashiriki kumbukizi ya Mkapa, azungumzia chanjo ya corona

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Rais Samia Suluhu Hassan, ameshiriki katika Kongamano la Kumbukizi ya Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa.

Akizunguza kwenye kongamano hilo lililofanyika leo Jumatano Julai14, 2021, Rais Samia amesema hayati Mkapa alitoa fursa zaidi kwa sekta binafsi na kukaribisha uwekezaji kutoka nje ya nchi.

“Hayati Mzee Mkapa alitoa fursa zaidi kwa sekta binafsi na kukaribisha uwekezaji kutoka nje. Hatua hizi zilisaidia kuongeza mapato ya serikali kutoka Sh bilioni 331.2 kwa mwaka 1995 hadi kufikia Sh trilioni 2 kwa mwaka 2005.

“Mzee Mkapa alifanikiwa kupunguza deni la taifa kutoka asilimia 143.7 ya pato la taifa tulilokuwa tukidaiwa mwaka 1995 hadi asilimia 60.7 mwaka 2005 na hii ni baada ya kuzishawishi nchi wahisani na taasisi za kifedha za kimataifa kutusamehe madeni.

“Hii iliwezekana baada ya kutumia uwezo wake wa diplomasia kuzishawishi taasisi za kifedha za kimataifa na nchi wahisani kusamehe madeni kutumia mpango wa HIPC (Heavily Indebted Poor Countries) uliosimamiwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la IMF. Mzee Mkapa alifanikiwa kupunguza deni la taifa kutoka asilimia 143.7 tuliyokuwa tukidaiwa mwaka 1995 hadi asilimia 60.7 mwaka 2005,” amesema Rais Samia.

Aidha, amefafanua kuwa: “Mzee Mkapa alianzisha taasisi nyingi ikiwemo TRA, PCCB, TASAF, NHIF, TANROADS, Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC), Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), MKURABITA, Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na nyingine nyingi.

“Sifa nyingine ya Mzee Mkapa ni uwezo wake mkubwa wa kutokuogopa mijadala ya kimataifa, miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000 kulikuwa na vuguvugu la kupinga masuala ya utandawazi, yeye hakufuata mkumbo badala yake alijitokeza hadharani kuutetea,” amesema Rais Samia.

Kuhusu virusi vya corona Rais Samia amesema kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na janga hilo hapa nchini.

“Serikali tunaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na Covid-19, ambapo kwa sasa tunakamilisha taratibu za kuagiza chanjo kwa ajili ya kinga, mwelekeo ni kwamba kila atakaye hitaji huduma ya chanjo iwe inapatikana, chanjo hiyo ni hiari,” amesema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,740FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles