30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wawakilishi CUF kwenda mahakamani

ZIFF chief guest, 1st vice president, Maalim Seif Sharif at ZIFF 2013NA HASSAN HAMAD (OMKR), PEMBA

MGOGORO wa uchaguzi visiwani Zanzibar umeingia katika sura nyingine baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kusema kuwa watakwenda mahakamani kuzuia kuchaguliwa kwa wawakilishi na madiwani wengine.

Alisema hawataruhusu viongozi wengine wa ngazi hizi kuchaguliwa tena kwa vile tayari wawakilishi na madiwani wateule wa CUF wamechaguliwa kihalali na wananchi na kukabidhiwa hati zao za ushindi baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, kwenye  viwanja vya Nngoma Hazingwa, mjini Chake Chake, kisiwani Pemba wakati akizungumza na viongozi wa wilaya, majimbo na jumuiya za chama hicho.

“Tutakwenda mahakamani kutetea nafasi zao na kutoruhusu viongozi wengine wa ngazi hizi kuchaguliwa tena kwa vile wanavyo vielelezo vyote vya kuchaguliwa,” alisema Maalim Seif ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar.

Alisema matokeo ya uchaguzi yaliyobandikwa kwenye vituo vya kupigia kura na kuthibitishwa na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo, majimbo 18 ya uchaguzi kisiwani Pemba yalichukuliwa na CUF pamoja na wadi zote 32.

Katika hatua nyingine, Maalim Seif aliyegombea urais kwa tiketi ya CUF, amewapa matumaini wafuasi wa chama hicho kuwa atatangazwa mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana na hatimaye kuiongoza Zanzibar.

Alisema kinachofanywa na watawala ni kuchelewesha kumtangaza, lakini hakuna namna yoyote CCM kuendelea kuongoza Zanzibar.

Maalim Seif alisema jumuiya na waangalizi wa kimataifa wote walisema uchaguzi ulikuwa huru, haki na wa uwazi.

Alisema kamwe chama chake hakitashiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles