29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Watumishi wa Umma wahimizwa kufanya kazi kwa weledi

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu, Balozi, Dk. Pindi Chana amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi, ufanisi na kuzingatia taratibu na kanuni zilizopo kwa mujibu wa sheria ili kutoa huduma bora kwa umma.

Pindi ametoa kauli hiyo Machi 19, 2022 katika Ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Njedengwa, Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha  Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo na kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Waziri mkuu kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 na makadirio ya bajeti mwaka 2022/ 2023 ambapo aliwahimiza kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na kuhudumia umma kama inavyokusudiwa na Serikali.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akitoa salamu katika uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika Ukumbi wa Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC) Machi 19, 2022 jiini Dodoma.

Alisema kwamba lengo la kuanzishwa kwa mabaraza ya wafanyakazi ni kuongeza ufanisi na tija katika sehemu za kazi, waajiri na wafanyakazi kubadilishana mawazo na kubaini mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

“Baraza hili linazinduliwa kwa mara ya kwanza hivyo kukutana kwenu hapa iwe sehemu muhimu kwenu ya kuibua ubunifu katika mipango yenu na utekelezaji wa shughuli za ofisi kwa kutumia rasilimali zilizopo tuone namna gani tunaweza kubuni mambo mbalimbali katika mipango yetu kuhakikisha umma unapata huduma stahiki na kwa wakati,” amesema Pindi.

Pia aliwapongeza kwa utendaji mwema wa kazi pamoja na ushirikiano hali inayosaidia shughuli za serikali kufanyika kwa wakati na viwango vinavyoridhisha katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Nimefarijika kuona upendo na mshikamano uliopo kati ya Menejimeti na wafanyakazi wote wa ofisi hii Idara zote na upande wa sera kwa kweli nawapongeza sana na moyo huu wa kazi mlionao unajenga heshima ya Ofisi ya Waziri Mkuu ninawapongeza sana na Mheshimiwa Waziri Mkuu anatambua tuko hapa na amewapongeza sana,” amepongeza Pindi.

Katibu Mkuu Ofsi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. John Jingu akieleza jambo kabla ya uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo katika Ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC) Machi 19, 2022 jiijini Dodoma.

Hata hivyo, Waziri Pindi aliwahimiza watumishi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kubadilika kifikra katika utendaji wa kazi akisisitiza upendo, bidii ya kazi, uwajibikaji na uadilifu kulingana na dira ya Ofisi hiyo ya kutoa huduma bora kwa umma na kufikia malengo ya serikali kwa kuratibu  sekta zote kwa ufanisi na tija.

“Tuepuke kufanya kazi kwa mazoea kwa upande wa Menejimenti tunatakiwa kujipanga ipasavyo kusimamia upatikanaji wa haki za wafanyakazi na wafanyakazi kuzingatia wajibu wao  kwa sababu suala la haki za wafanyakazi ni muhimu sana tukalipa kipaumbele,” ameeleza.

Wakati huohuo aliitaka Menejimenti kutataua kero za wafanyakazi kwa wakati hatua itakayosaidia kuleta mabadiliko katika maisha yao na ajira kwa ujumla na kuhakikisha wanakuwa na vitendea kazi vya kutosha vitakavyowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kufanya kazi kwa kujituma.

“Vivile tuna wajibu wa kutatua kero za wafanyakazi kwa wakati kuleta mabadiliko ya maisha na ajira zao  na ili yote haya yatimie ni muhimu uongozi utoe umuhimu mkubwa katika kipaumbele  kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi vya kutosha hususani katika  bajeti hii ambayo ninaamini mtaijadili na kuweka vipaumbele vinavyotekelezeka,”alifafanua Pindi.

Aidha uzinduzi wa Baraza hilo uliambatana na uchaguzi wa Katibu na Katibu Msaidizi ambapo, Janet Shija alishinda nafasi ya Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu huku Edwald Bonafasi alishinda nafasi ya Katibu Msaidizi wa baraza hilo linaloongozwa na Mwenyekiti wake, Dk. John Jingu na Mwenyekiti Mwenza akiwa ni Kaspar Mmuya.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga alipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akitimiza mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Pombe Magufuli aliyefariki Machi 17, 2021 akisema amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles