29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

MAUWASA yatekeleza miradi ya Bilioni 1.3

Na Samwel Mwanga, Maswa

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Maswa (MAUWASA) iliyoko Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imetekeleza miradi mitano ya maji kwa gharama ya Sh Bilioni 1.3 kwa kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa, Mhandisi Nandi Mathias ameeleza hayo wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari juu ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo mingine inaendelea kutekelezwa na mingine ikiwa imekamilika.

Moja ya mradi wa maji ambaonunatekelezwa na MAUWASA.

Amesema kuwa Mamlaka hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali kwa lengo la kuboresha huduma ya maji katika maeneo wanayoyahudumia.

Amesema upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa maeneo yanayohudumiwa na Mamlaka hiyo umeongezeka kutoka asilimia 74 hadi asilimia 84 kwa kipindi hicho.

Mhandisi Nandi amesema kuwa miradi ambayo imetekelezwa kwa kipindi hicho ni pamoja na ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji lita milioni moja, ununuzi wa dira za maji, ujenzi wa chujio la maji, kuongeza mtandao wa maji kupitia fedha za Uviko-19 na gharama za umeme.

Amesema Mauwasa imekuwa ukitekeleza miradi hiyo kwa kufuata lengo la Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutekeleza miradi hiyo ni kutaka kuhakikisha wananchi wanaohudumiwa na Mamlaka hiyo wanapata maji ya kutosha yaliyo safi na salama.

“Maji ni lazima yatoshe na ndio sababu ya Rais Rais Samia Suluhu kuanzisha kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani na kazi hiyo sisi Mauwasa ndiyo tunayoifanya kwa sasa kupitia miradi mbalimbali,” amesema Mhandisi Nandi.

Amefafanua kuwa gharama za kila mradi kuwa ujenzi wa tenki ni Sh milioni 350, ununuzi wa dira za maji 2,000 Sh milioni 52 na ujenzi wa ukamilishaji wa chujio la maji katika bwawa la New Sola Sh milioni 562.12.

Amesema miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa Ustawi wa Taifa kwa Maendeleo katika kupambana na Mmaambukizi ya UVIKO-19  Sh 246,467,204 na gharama za kulipia deni la umeme kwenye mitambo ya kusukuma maji kwenye Bwawa la New Sola Sh milioni 100.

Mhandisi Nandi amesema kuwa miradi iyo mingi inayotekelezwa na Mamlaka hiyo wamekuwa wakitumia Wakandarasi na Wataalam wake wa ndani kwa njia ya Force Akaunti.

Mauwasa imekuwa ikiwahudumia wananchi wapatao 174,000 katika mji wa Maswa na vijiji vipatavyo 11 katika wilaya hiyo ambavyo ni Zanzui, Mwabayanda, Mwashegeshi, Dodoma, Malita, Nghami, Iyogelo, Buyubi, Mwasita, Hinduki na Mwadila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles