28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi wa afya waliotafuna fedha wapewa siku saba

Na Derick Milton, Simiyu

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Miriam Mmbaga ametoa muda wa siku saba kwa Mganga Mkuu wa mkoa huo kupatiwa majina ya watumishi wa vituo vya kutolea huduma za Afya mkoa mzima ambao wanadaiwa kutafuna fedha za makusanyo kwenye vituo vyao.

Mmbaga ametoa maagizo hayo leo Januari 5, wakati akiongea na watumishi wa idara hiyo Halmashauri ya mji wa Bariadi na Bariadi vijijini pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwenye kikao kazi.

“Mimi sina utani wala urafiki na mtu ambaye ni mbadhirifu wa fedha za umma, ndani ya siku saba RMO niletewe majina ya watumishi hao, lakini Kwanza wazirejeshe ndani ya muda huo, na hatua kali zitafuata dhidi yao,” amesema Mmbaga.

Hatua hiyo imekuja baada yakupewa taarifa na Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa, Dk. Hamis Kulemba juu ya uwepo matumizi mabaya ya fedha za makusanyo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Dk. Kulemba amemweleza Katibu Tawala huyo kuwa wamebaini baadhi ya vituo vya kutolea huduma, makusanyo hayajapelekwa benki na wahusika wakiwauliza wanasema kuwa wamezitumia.

“Kuna baadhi ya vituo tumevitembelea, makusanyo yapo, ukiangalia akaunti ni sifuri, ukiwauliza wanasema wamepelekwa kwenye akaunti zao binafsi, wengine wanasema wamezitumia,” amesema Dk. Kulemba.

Hata hivyo, Dk. Kulemba ameongeza kuwa katika mkoa huo kuna changamoto kubwa ya matumizi mabaya ya mfumo wa utoaji dawa kwa wagonjwa hali ambayo imesababisha vituo vingi kutokuwa na fedha za kutosha.

“Kuna baadhi ya vituo tumevitembelea, makusanyo yapo, ukiangalia akaunti ni sifuri, ukiwauliza wanasema wamepelekwa kwenye akaunti zao binafsi, wengine wanasema wamezitumia,” amesema Dkt Kulemba.

Hata hivyo Dk. Kulemba ameongeza kuwa katika mkoa huo kuna changamoto kubwa ya matumizi mabaya ya mfumo wa utoaji dawa kwa wagonjwa hali ambayo imesababisha vituo vingi kutokuwa na fedha za kutosha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles