24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Watuhumiwa 48 mbaroni Morogoro

Na Ashura Kazinja, Morogoro

JESHI la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watuhumiwa 48 wa makosa mbalimbali ikiwemo wizi wa mafuta ya dizeli, simu za mkononi 85 na kompyuta 6 zenye program ya kuflashi simu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, alisema jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa hao 48 kwa makosa mbalimbali likiwemo kosa la kukutwa na mafuta ya dizeli lita 1,240, mipira miwili ya kunyonyea  mafuta ya wizi, mitambo ya kutengeneza pombe ya gongo na simu za mkononi 85.

Kamanda Mutafungwa alisema katika oparesheni ya kudhibiti matukio ya wizi wa simu za mkononi, kwa kushirikiana na kitengo cha makosa ya wizi kwa njia ya mtandao, wamefanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 41 wa matukio mbalimbali ya wizi wa simu.

Alisema mbali na simu 85, pia walifanikiwa kukamata kompyuta sita zikiwa na program za kuflashi simu, na pikipiki nne zilizokuwa zikitumika  katika matukio ya uporaji wa simu.

“Agosti 14 hadi 30 tumefanya oparesheni ya kudhibiti matukio ya wizi wa simu za mikononi, uporaji wa simu kwa kutumia pikipiki, wizi wa simu katika kumbi za starehe katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Morogoro na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 41 wakiwemo watuhumiwa 12 wazoefu ambao ni mafundi wanaobadilisha Imei na kuflash simu za wizi,” alisema Mutafungwa.

Akiwataja watuhumiwa hao alisema ni Amon Mapunda, ambae anafanya shughuli za kuflashi simu nyumbani kwake mtaa wa Kididimo Manispaa ya Morogoro, Paul William, na  Abbas Hassan anae fanya shughuli zake katika mtaa wa Msamvu.

Aidha aliwataja waendesha bodaboda ambao ni waporaji simu wazoefu  kuwa ni Emmanuel Massawe(Madega), Mohamedi Omari (Mudi dundo), Ally Chombo, Kelvin Maliki (Lotiloti), huku akiwataja wapokeaji na wauza simu hizo kuwa ni Mengi Selemani, Said Hamis.

Hata hivyo aliyataja baadhi ya maeneo ambayo wahalifu hao walikuwa wakifanya matukio yao ya uporaji kuwa ni klabu za usiku za maeneo ya Msamvu, Chamwino, Nanenane, Kigurunyembe, Mafiga na maeneo yenye mikusanyiko ya watu hasa sehemu za minada, masoko na katika vyuo vikuu.

Katika tukio la wizi wa mafuta alisema Agosti 29, majira ya saa 6 usiku katika kitongoji cha  Miembeni Kata ya Berega wilayani Kilosa, askari polisi walipokea taarifa za watu wakiwemo madereva wa malori ya mafuta kushiriki wizi wa mafuta ya kampuni ya state oil yenye makao yake Mdaula-Chalinze mkoa wa Pwani yakiwa yanasafirishwa kwenda nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles