25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 17, 2022

‘Asilimia 99 ya watoto wanapata chanjo nchini’

Na DERICK MILTON-MWANZA

MKURUGENZI wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Dk. Leornald Subi, amesema utolewaji wa chanjo kwa watoto wachanga na wenye umri chini ya miaka mitano nchini, kimeongezeka kutoka asilimia 94 mwaka 2014/15 hadi asilimia 99 mwaka 2020.

Alisema asilimia moja iliyobaki inarudisha nyuma juhudi za Serikali za kuwalinda watoto na magonjwa hatarishi.

Dk Subi alisema hayo wakati akifungua mafunzo ya kwa waandishi wa habari ya siku moja mkoani Mwanza juu ya elimu ya Chanjo.

Dk. Subi alisema mafanikio hayo ya kuongeza utolewaji wa chanjo, yametokana na Serikali ya awamu ya tano kuendelea kuboresha kitengo cha chanjo kwa kuongeza bajeti ya chanjo kutoka Sh. Bilioni 10 mwaka 2014/15 hadi bilioni 30 mwaka 2020.

Alisema mbali na Serikali kuongeza bajeti ya chanjo, maboresho makubwa yamefanyika kwenye maghala ya kuhifadhi chanjo, ambapo ukarabati wake umeghalimu zaidi ya bilioni 1.3 na kuboresha vyumba vya ubaridi (friji) ambavyo vimegharimu Sh milioni 450.

Alisema Serikali imenunua magari 74 ya kusambaza chanjo nchi nzima yenye thamani ya Sh bilioni 7.7, ambapo malengo ya maboresho hayo ni kuhakikisha kiwango cha utolewaji wa chanjo kwa watoto kinaongezeka na kuwa bora zaidi.

“ Juhudi hizi zimesababisha baadhi ya magonjwa kutokomea kama polio, pepopunda kwa watoto wachanga, wodi za magonjwa ya surua kwa sasa hakuna, lakini magonjwa ya kuharisha nayo hakuna kwa sasa, haya magonjwa yalikuwepo zamani miaka 1999, lakini leo hakuna,” alisema Dk Subi.

Hata hivyo Dk. Subi aliwataka waganga wakuu wa mikoa nchi nzima, kuhakikisha wanawafuatilia na kuwapata watoto wote ambao wanahaki ya kupata chanjo, wanawapata ili waweze kupatiwa chanjo.

Alisema asilimia moja ambayo imebaki ya watoto ambao hawajafikiwa na chanjo, wanatakiwa kutafutwa kwenye maeneo yao ili kuweza kufikia malengo ya Serikali ya kuhakikisha chanjo inatoa kwa asilimia 100.

Aidha aliwataka wazazi na walezi wa watoto wachanga na wale wenye umri chini ya miaka mitano ambao bado hawajawapeleka watoto wao kupata huduma hiyo, kuhakikisha wanawapeleka kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wapate chanjo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,717FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles