24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 6,800 wameathirika kwa mabusha, matende

paul-makonda NA HADIA KHAMIS-DAR ES SALAAM

WATU 6,800 jijini Dar es salam wameathirika kwa magonjwa ya matende na mabusha, MTANZANIA limeelezwa.

Kiwango hicho ni kikubwa kwa wakazi wa Dare s salaam kwani hadi sasa Watanzania bilioni 2.7 wameathirika na magonjwa yasiyopewa kipaumbele ikiwamo ngirimaji na matende hususani vijijini.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa dawa za kinga tiba ya matende, minyoo na mabusha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, alisema kuwa alisema zoezi la utoaji wa dawa za kinga tiba zitatolewa bure ambapo zaidi ya Watanzania milioni 4.5 wanatarajiwa kupata kinga ya tiba hizo.

 “Kinga tiba imeanza kutolewa jana Oktoba hadi 29, mwaka huu kwa watu wenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea  kwa kumeza dawa za Mectizan na Albendazole za kukinga na kutibu magonjwa ya minyoo tumbo, mabusha na matende,” alisema Makonda.

Makonda alisema dawa hizo ni salama na zimethibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambapo aliwataka viongozi kuwashawishi wananchi kushiriki zoezi hilo.

Alisema magonjwa yasiyopewa kipaumbele yameathiri sehemu kubwa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kusababisha ulemavu na kupunguza uwezo wa wananchi kushiriki katika shughuli mbali mbali za ujenzi wa taifa.

Pamoja na mambo mengine, Makonda alisema hadi sasa Watanzania 100,000 nchi nzima wameathirika na vikope, 25,000 wameathirika na mabusha na 10,000 wameathirika na matende.

“Kinga tiba zinasaidia kukinga upungufu wa damu, kumuepusha mtu kupata upofu, kupunguza maambukizi kutoka kwa mtu mmoja mmoja kwenda kwa mwingine, kuua vimelea vya magonjwa hayo, kukinga na kupunguza maumivu na madhara yanayosababishwa na magonjwa hayo pamoja na kupungua kwa magonjwa ya ngozi,” alisema.

Akizungumza katika zoezi hilo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Grace Magembe alisema hadi sasa tayari watu 104 kwa Mkoa wa Dar es Salaam wameshafanyiwa upasuaji wa mabusha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles