Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Nyota walioshiriki mashindano hayo ni kutoka katika klabu zote za Tanzania na wengine nchi za Uganda, Rwanda, Kenya na Burundi.
Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza kwa watoto ambao wamecheza viwanja 18 Hafidhi Twalibu aliyeshinda kwa pointi 46, wa pili ni Stanley Emilias amepata pointi 45 huku Sabrina Juma akiwa mshindi wa tatu na pointi 22.
Wengine ambao wamecheza viwanja tisa, mshindi wa kwanza ni Frank Emmanuel pointi 49 wa pili Joseph Msaada amepiga pointi 50 huku nafasi ya tatu ni Ellah Muga ameshinda pointi 68.
Akizungumzia ushiriki huo wa vijana wadogo, leo Agosti 03,2024, Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo, Meja Jenerali Ibrahim Mhona ameipongeza benki ya KCB kwa kuchukua hatua ya kushirikisha watoto katika mashindano hayo makubwa.
Mhona amesema licha ya kuwa mchezo wa gofu haujapiga hatua sana hapa nchini lakini klabu ya Lugalo inasonga mbele kwa kuhakikisha inaanda timu ya siku zijazo.
“Pongezi kwa watoto ambao wamefanya vizuri na kupatiwa zawadi zao, wachezaji wasiofanya vyema wakati ujao watafanya vizuri katika mashindano mengine.
Aidha Mhona amewapongeza wazazi kwa kuwaruhusu watoto kucheza mchezo wa gofu .
Naye, Nahodha wa watoto (Juniors), Ally Kayombo ameyaomba makampuni mengine kujitokeza kudhamini mashindano ya watoto kwa lengo la kuendelea vipaji vyao.
“Ombi letu kwa makampuni mengine kama KCB kujitokeza kudhamini mashindano kama ili watoto washirikii au kuandaa mashindano ya vijana,” amesema.
Nahodha huyo amesema mashindano ya awamu hii wameboresha zawadi tofauti na miaka iliyopita, kitendo kinachoongeza chachu ya kuongeza bidii.