23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

TTCL yaleta huduma za kidigitali kwa wakulima katika maonesho ya Nanenane

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limewasilisha huduma mbalimbali katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane mwaka huu, zilizolenga kuwasaidia wakulima hasa wale wanaolima kisasa kwa kutumia teknolojia.

TTCL imepeleka huduma ya mawasiliano imara ambayo itawarahisishia wakulima kuwasiliana na kufuatilia masoko duniani kupitia huduma ya intaneti.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo, Agosti 3, 2024, katika maonesho hayo yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, Afisa Uhusiano wa TTCL, Ester Mbanguka, aliwaomba wakulima kutumia huduma ya mtandao ili kuboresha kilimo na kuendana na teknolojia.

“Tumewaletea mifumo ya teknolojia kwa wakulima na wale ambao sio wakulima, kwani sasa hivi dunia yote ipo kidigitali. Watakapofanya kilimo ni lazima wauze au watafute pembejeo za kilimo, na wanapokuwa na huduma ya mtandao wanaweza kuwasiliana na wauzaji wa pembejeo na wanunuzi wa mazao yao kwa njia rahisi,” alisema Ester.

Ester aliwataka wateja wa TTCL kote nchini kutoa taarifa kwa kituo cha huduma kwa wateja pindi wanapokumbana na changamoto yoyote wanapotumia huduma zao ili ziweze kutatuliwa kwa wakati na sio kulalamika sehemu tofauti.

“Nitoe rai kwa wateja wetu wote nchini kuripoti kwa kituo cha huduma kwa wateja pindi wanapopata changamoto katika huduma zetu ili tuweze kuwasaidia haraka. Wanapozungumza pembeni wanabaki na tatizo na sio kutatua tatizo,” alisema.

Aliongeza kuwa katika maonesho hayo wamepata wateja wapya wa huduma ya intaneti ambao ni waoneshaji, na pia wamefunga intaneti ya bure kwenye banda lao ambapo watu wanaweza kuipata bila malipo. Vilevile, wameweka huduma hiyo katika baadhi ya maeneo kwenye maonesho kwa ajili ya wananchi wanaotembelea maonesho hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles