23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WATOTO WA RAY, RAYVANNY WALIVYOTIKISA

Na CHRISTOPHER MSEKENA

WATOTO wa mastaa wa filamu na muziki Bongo, Jaden na Jaydan wiki hii wamegonga vichwa vya habari za burudani kufuatia matukio waliyoyafanya wazazi wao.

Jaden ambaye ni mtoto wa waigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hansi, alitikisa mitandao ya kijamii kwa picha zake kali zenye mvuto mkubwa zilizotolewa na wazazi wake wakati wakisheherekea siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake, Januari 21 mwaka huu.

Kadharika, Jaydan ambaye ni mtoto wa msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na video vixen, Fahyma alitikisa mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kwenye picha na wazazi wake walipokwenda kusalimia wazazi jijini Mbeya.

Kuna vitu vingi ambavyo Swaggaz tumeviona vinavyofanya Jaden na Jaydan wafanane mithili ya mapacha. Hebu cheki mambo haya..

MAJINA YA BABA ZAO

Wakati baba yake Jaden akiwa ni Ray, baba wa Jaydan ni Rayvanny. Majina ya baba wa watoto hawa yanafanana herufi tatu za mwanzo  (Ray), wote wanaitwa Ray.

MAJINA YAO SASA

Lakini hata majina yao yanafanana na usipokuwa makini unaweza kuwachanganya kwani mtoto wa Ray anaitwa Jaden na mtoto wa Rayvanny anaitwa Jaydan.

Herufi mbili za mwanzo za majina yao zinafanana (Ja), yote yanaanzia na Ja.

WATOTO WA MASTAA

Inafahamika wazazi wa Jaden ambao ni Ray na Chuchu  ni waigizaji mahiri wa filamu hapa Bongo na kazi hiyo imewapa umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania.

Kwa upande wa pili, wazazi wa Jaydan ni watu maarufu pia kwenye muziki. Rayvanny ni mwanamuziki huku Fahyma ni mrembo aliyejipatia ustaa baada ya kuonekana kwenye video za muziki.

WOTE NI VIDUME, WEUPE

Watoto hawa, Jaden na Jaydan wote ni wa kiume tena wana rangi nyeupe jambo linalofanya waendelee kufanana mithili ya mapacha tena wa baba na mama mmoja.

Si hivyo tu bali hata kuzaliwa wote walizaliwa mwaka jana ambapo, Jaden alizaliwa Januari 21 na Jaydan alizaliwa Aprili 17.

NI UZAO WA KWANZA

Jaden ni mtoto wa kwanza kwa mwigizaji Ray na mtoto wa pili ya Chuchu Hansi huku Jaydan ni mtoto wa kwanza kwa mwimbaji Rayvanny na  Fahyma.

PHOTOGENIC BOYS

Hawa ni watoto wenye mionekano mizuri ya picha yaani photogenic. Unaweza kuthibitisha hilo ukitazama picha ya Jaden zilizotoka wiki hii ambazo zimewapagawisha mastaa wakubwa kama Mange Kimambi, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Jacqueline Wolper na wengine kibao.

Lakini pia Jaydan, naye yupo vizuri kwenye picha, ana mwonekano wa picha na ukitembelea ukurasa wake wa Instagram utaona dogo anavyokimbiza kwa picha kali ambazo zimefanya ajizolee wafuasi zaidi ya laki 1.4 kwenye page hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles