23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto 270 kupoteza maisha kila mwaka kwa lishe duni

Na Mwandishi wetu, Dodoma

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis, amesema zaidi ya watoto milioni 2.6 wenye umri chini ya miaka mitano wamedumaa na zaidi ya watoto 270 wa umri huo hupoteza maisha kila mwaka kutokana na lishe duni.

Akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa habari kuhusu programu Jumuishi ya malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto leo Desemba 10,2021, Jijini Dodoma,Mwanaidi amesema mikoa inayongoza kwa upatikanaji wa chakula ndiyo ina changamoto hiyo ya lishe.

“Tanzania ni moja kati ya nchi za Afrika yenye idadi kubwa ya watoto wenye utapiamlo. Idadi kuwa ya watoto hao ni katika mikoa ya Dar es Salaam, Kagera, Kigoma, Mara, Dodoma, Geita, Tanga, Ruvuma, Mbeya, Morogoro na Tabora,tukumbuke baadhi ya mikoa hii ina kiwango cha juu cha upatikanaji wa chakula, programu hii inalenga kuchangia katika kumaliza changamoto ya lishe kwa watoto wetu nchini” amesema Mwanaidi.

Amesema hivi sasa malezi na makuzi ya watoto hususani wa chini ya miaka nane, yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukatili, unyanyasaji, lishe duni na wazazi na walezi kufuatilia mienendo na usalama wa watoto.

Ameongeza kuwa, Serikali na wadau mbalimbali wanaendelea na juhudi za kuhakikisha watoto wote wanakuwa na usawa katika malezi na makuzi pamoja na kuvisimamia vituo 5274 vya malezi ya watoto.
Aidha, vituo 1481 vimeanzishwa na mwaka 2021 Serikali imejenga vituo 20 mkoani Dodoma na vituo 10 Dar es Salaam, 10 vimeandaliwa kuwawezesha watoto chini ya miaka mitano kupata malezi na uchangamshi wa awali.

Ameongeza pia vitendo vya ukatili kwa watoto vinarudisha nyuma jitihada za Serikali na wadau kuhakikisha watoto wanakua katika utimilifu wao akitaja kuwa kwa miezi tisa kumekuwa na matukio zaidi ya 6009, hivyo waandishi wana nafasi kubwa kushirikiana na Mamlaka nyingine kuelimisha jamii ili iweze kubadilika.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Mwajuma Magwiza amesema Waandishi wa Habari ni kundi muhimu katika kupeleka taarifa kwa jamii ikiwa wataelimishwa kwani wao pia ni sehemu ya utekelezaji.

“Tunaamini kundi hili likipata uelewa sahihi wakati huu, hata kwenye utekelezaji inakuwa kazi rahisi, Programu hii itazinduliwa tarehe 13 mwezi huu na kawaida ya Wizara huwa tunaanza kujenga uwezo kwa makundi muhimu ambayo yanatakiwa kupelekwa taarifa sahihi,”amesema

Naye mmoja wa waandishi hao, Jaliwasom Jasson ameshukuru kwa kupata elimu na kujengewa uwezo wakati wote wa utekelezaji wa masuala ya watoto na kuahidi kuendelea kufanya vema zaidi katika programu hiyo ya malezi na makuzi kwa kiwango na matokeo makubwa kwa kushirikiana na Serikali.

“Tunapokwenda kuitekeleza programu hii tunaomba tushirikishwe katika mikoa yote tukitumika vizuri nina uhakika elimu hii itawafikia jamii na kuwekeza vizuri kwa watoto wetu,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles