27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Watoa huduma za Posta watakiwa kuwa wabunifu

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi amewapa maagizo matatu watoa uduma za Posta ikiwemo kuleta ubunifu wa nini cha kufanya ili kuboresha huduma hizo nchini.

Maagizo mengine ni kuwa mabalozi wazuri wa sekta ya posta pamoja na kupeleka mapendekezo ya kile ambacho kimefanyika katika sekta hiyo.

Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 7,2021, jijini Dodoma wakati akifungua warsha ya watoa huduma za Posta, Dk. Yonazi amesema mkutano huo ni muhimu hivyo amewapa maagizo ya kuleta ubunifu nini cha kufanya ili kuboresha huduma za posta nchini

Pia ameyataja Maagizo mengine ni kuwa mabalozi wazuri wa sekta ya posta pamoja na kupeleka mapendekezo ya kile ambacho kimefanyika katika sekta hiyo.

“Posta ni sekta muhimu sana inawezesha bidhaa moja kutoka sehemu moja mpaka nyingine na usafirishaji wa mizigo bado unabaki kuwa ni kitu muhimu serikali imefanya jitihada kubwa na imewekeza kuhakikisha miundombinu inakuwa rafiki.

“Na  tumeweka Postikodi katika Halmashauri 21 na mipango inaendelea kuendelea kuweka katika maeneo mengine hii itasaidia mizigo kufika kila mahali,” amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk.Jabir Bakari amesema warsha hiyo ni muhimu kwani watoa huduma hao wamekuwa wakitoa huduma ya kusafirisha mizigo kutoka eneo moja mpaka jingine.

Amesema kwa kutumia mkutano huo watajadiliana ni changamoto zipi wamekuwa wakikutana nazo na kisha kuzitafutia ufumbuzi.

“Pia tupo hapa kuona teknolojia inatusaidiaje kutoka katika hili wimbi la Uviko-19 kwa kuongeza ufanisi katika eneo la posta.Tupo katika mwelekeo mzuri kutumia sekta ya posta tunatembea vizuri tunataka kuongeza kasi zaidi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles