31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Alikiba azindua albamu yake ya tatu Only One King

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Usiku wa kuamkia leo October 7,2021 Msanii wa Bongo Fleva, Ali Salehe Kiba amefanya Listening Party na kuzidunzi rasmi wa album yake ya miongoni mwa nyimbo zilizopo kwenye Albamu hiyo inayofahamika kama ONLY ONE KING yenye nyimbo 16.

Baadhi ya Wasanii wa Bongo Fleva waliokuwepo kwenye usiku huo akiwamo Nandy (Katikati), Dayna Nayange(Kulia).

Alikiba amezindua albamu yake ya 3, katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Hoteli Dar es Salaam ambapo ndani yake ina nyimbo 16 kwenye albamu hiyo, Kiba amewashirikisha wasanii wa lebo yake ya Kings Music, na wengine wa ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo AliKiba amesema albamu yake imeandaliwa na mzalishaji wa kazi za wasanii (Produce) mmoja tu Yogo on the beat na kumshukuru kwa uvumilivu na kuwea kufanya kazi nzuri.

Alikiba amesema amefanya collabo na Patoranki kutoka Nageria ambaye pia alikuwa miongoni mwa wasanii waliohudhuri kwenye usiku huo na kutumbuz=iza pamoja wimbo huo unaofahamika kama Bwana Mdogo.

Msanii Pantoraking(Kulia) akisalimiana na Rich Mavoko(Kushoto).

Aidha, mbali na Pantoranki, Alikiba pia amewashirikisha kundi la Sauti Sol kutoka Kenya, Sarkodi, Blaq Diamond, Mayorkum, Nyanshiski pamoja na vijana wa lebo yake ya Kings Music.

“Sababu za kutokufanya collabo na wasanii wa Tanzania zaidi ya vijana wangu wa Kings Music ni kutokana na kukosa muda hivyo ndio maana nikashindwa kushirikisha hata wasanii wa Hip hop lakini naahidi katika albamu ijayo nitashirikiana na wasanii wa ndani.

“Hivyo wanawashukuru Kings Music kwa kuwa wanamchango mkubwa sana katika kukamilisha albamu yangu kwani tulikuwa tkisaidiana hata kwenye utunzi hasa msanii Tommy Fravour,”amesema Alikiba.

Miongoni mwa nyimbo zilizopo kwenye albamu hiyo inayofahamika kama ONLY ONE KING ni pamoja na Amour, Let me, Tamba, Sitaki Tena, Washa, Bwana Mdogo, Niteke, Oya Oya, Utu, Jealous, Habibty, Gimme Dat, Ndombolo, Happy

Patoranki amempongeza Alikiba kwa kufanya albamu nzuri nakusema wimbo ambao ameupenda zaidi ni ‘Niteke uwe na mimi’ huku akiuimba kwa mara ya kwanza na kutaka urudiwe tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles