27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

WATEJA BENKI YA UBA KUPATA HUDUMA SAA 24

Na FARAJA MASINDE -DAR ES SALAAM

BENKI ya United for Afrika (UBA), imezindua kituo cha mawasiliano kitakachowawezesha wateja wake kupata huduma na msaada kwa saa 24

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo nchini, Peter Makau alisema kufunguliwa kwa kituo hicho itakuwa ni nyenzo muhimu ya kuwa karibu na wateja wao na kujiimarisha zaidi katika utoaji wa huduma zake.

“Tunahama kwenye mfumo wa kuwasiliana na wateja wetu kwa saa 12 tu za kazi kama ilivyokuwa hapo awali na sasa wataweza kutupigia muda wowote na kupata msaada wa kibenki kwa saa 24.

“Moja ya mikakati yetu ni kuhakikisha kuwa tunatoa huduma bora zaidi kwa wateja hivyo kuwapo kwa kituo hiki cha saa 24 kitakuwa ni moja ya mikakati ya kutoa huduma bora, hivyo wateja wanaweza kuwasiliana nasi pia kwa njia mbalimbali ikiwamo mitandao ya kijamii ya, Facebook na Twitter pamoja na barua pepe moja kwa moja,” alisema Makau.

Katika hatua nyingine, Makau alisema kwa sasa wanatarajia kufungua matawi mengine mwishoni mwa mwaka huu kwenye mikoa ya Dodoma na Mwanza, huku wakitarajia kufungua matawi mengine matatu jijini Dar es Salaam.

“Tutakuwa tukifungua matawi kila mwaka, kwa kuanza kabla ya mwaka huu kuisha tutakuwa tumefungua tawi Dodoma na mwakani tutahamia Mwanza na Mtwara, tunawakaribisha wananchi wote na hata wale ambao si wateja wetu na wangependa kujiunga na sisi wanakaribishwa,” alisema Makau.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles