30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania watakiwa kuwekeza sehemu za kihistoria

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Watanzania wameshauriwa kuwekeza katika sehemu ya historia ili kuweza kujiongezea kupato.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu makumbusho ya Taifa, Dk. Noel Lwoga wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya wafanya biashara.

Amesema ni vyema kwa Watanzania kutumia fursa hizo kwa kuwekeza katika majengo ya kihisitoria.

“Katika maeneo ya mali tunatoa huduma nyingi ya malazi,hoteli ni vyema kwa wananchi wa karibu kuwekeza kwa kujenga migahawa katika maeneo hayo,” amesema Dk. Lwoga.

Aidha, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya filamu ya Royal Tour kwani imewaongezea kipato kwa asilimia kubwa.

Amesema kwasasa wanampango wa kuboresha huduma za makumbusho ili yaweze kuwa ya kidigital.

“Tukiboresha katika makumbusho yetu tutaweza kupata wageni wengi sana na pato la Taifa litaongezeka,”amesema Dk. Lwoga.

Amefafanua kuwa kwasasa wameanzisha utalii wa ndani ya miji yaani Dar es Salaam City Tour.

Amesema jumla ya vivutio 18, vitatembelewa katika matembezi hayo.
Aidha alivitaja vituo hivyo, kuwa ni pamoja.

1.Makumbusho na nyumba ya utamaduni
2.Askari Monument
3.Clock Tower
4.Mnazi Mmoja.
5.Old Boma
6.St.Joseph Cathedral
7.White Fathers House
8.Old postal Office
9.Azania Front Church
10.Ferry Fish Market.
11.TINGATINGA Association group via Tanzanite Bridge
12.Village Museum
13.Kunduchi Ruins
14.Bustani ya kumbukumbu ya vita ya kwanza ya dunia 1914-1918
15.Ofisi ya kamati kuu ya(OAU committee) ukombozi wa kusini mwa Bara la Africa
16.State House/Ikulu
17.Ocean Road hospital
18.Botanical Garden
ambapo kiingilio ni Sh 15,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles