23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DC Ileje anusa upigaji wa Bilioni 1, ataka nyaraka za manunuzi

*Awataka Wahandisi wa Halmashauri kukaa mguu sawa

*aapa kula sahani moja na watakaobainika kugushi nyaraka

Na Denis Sinkonde, Songwe

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Anna Gidarya amesikitishwa na uzembe uliofanywa na Wahandisi wa Halmashauri hiyo kufuatia kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 1, hivyo ameapa kushughulika na watakaobainika kugushi nyaraka wakati wa kutekeleza miradi hiyo wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Anna Gidarya akitoa maelekezo.

Onyo hilo amelitoa leo Julai 10, 2022 baada ya kubaini kuwapo kwa madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango na kwa kutumia mbao zisizofaa katika shule ya Msingi Ipapa licha ya wilaya hiyo kuwa na utajiri wa misitu.

Aidha, mbali na madawati hayo pia amebaini kuwa hata madarasa yaliyojengwa katika shule hiyo ya Ipapa yameanza kutoa nyufa licha ya kwamba bado hayajaanza kutumika.

“Nimetembea na kuona madudu mengi katika miradi inayotekelezwa hapa, tumekagua madarasa mapya ambayo hayajaanza kutumika katika shule hii ya Ipapa tayari yana nyufa, kama hiyo haitoshi wilaya yetu ya Ileje inautajiri wa misitu ya mbao lakini chakusikitisha aina ya madawati yaliyotengenezwa yako chini ya kiwango na hayafai kabisa kutumika na watoto wetu.

“Hiyo pia ninachangiwa na aina ya mbao zilziotumika, hivyo kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya naagiza yasitumike, yatengenezwe mengine kwa gharama zenu. Naagiza miradi yote ikamilike kabla ya Julai 28, nataka mniletee nyaraka zote ambazo zimetumika kwenye hatua za ujenzi na michakato yote ya manunuzi na ole wenu mkibainika mmegushi nyaraka nitalala na nyie mbele,” ameonya Gidarya.

Aidha, Gidarya amewakumbusha Wahandisi wa Halmashauri kusimamia kwa ukaribu miradi inayojengwa wilayani humo ili itekelezwe kwa viwango na kuacha ubabaishaji ambao umekuwa ukifanyika.

Gidarya amesema katika miradi hiyo ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 1, Wahandisi wamekuwa ni changamoto katika usimamizi wa miradi na kuonya kuwa hawatavumiliwa kwani wanashindwa kuwajibika kwenye nafasi zao.

“Wahandisi wamekuwa hawafiki kwenye maeneo ya miradi kwa ajili ya kuwasimamia mafundi na hii ni chanyamoto ambayo imesababisha miradi mingi kutekelezwa tofauti na mipango iliyopangwa ikiwamo uwekaji wa vyoo vya alminium shule ya Ipapa na uwekaji wa fremu katika shile ya sekondari Chitete, haya yote tumeyabaini wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ilipokuwa ikikagua miradi hii,” amesema Gidarya.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Ileje, Pastori Mashiku amesema maelekezo ya kamati ya ulinzi na usalama ni ya msingi, huku akiagiza kila mtaalamu asimamie wajibu wake, nakumtaka Mhandisi na wasaidizi wake kufika maeneo ya miradi kufanya ukaguzi.

Awali, Diwani wa kata ya Isongole, Gwalusako Kapesa alisema ujio wa kamati utasaidia kuweka msukumo kwa Wahandisi kufika eneo la mradi na kubaini mapungufu ikiwepo madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango na kuwasimamia mafundi waliopewa kazi ya kujenga mradi wa shule ya msingi Ipapa.

Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa na kamati ya ulinzi na usalama ni ujenzi wa jengo la wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu(ICU) katika hospitali ya wilaya Ileje inayojengwa kwa thamani ya Sh milioni 250, ujenzi wa shule mpya kitongoji cha Ipapa Kijiji ha Isongole kata ya Isongole wilayani humo inayojengwa kwa Sh milioni 400, ujenzi wa shule ya sekondari ya wanawake kwa thamani ya Sh milioni 470.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles