Ramadhan Hassan,Dodoma
WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,imewataka Watanzania kuhakikisha wanajikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kufanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki,kula mlo unaofaa,kutotumia tumbaku na kupunguza matumizi ya pombe.
Hayo yalielezwa leo Mei 17 bungeni na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dk Faustine Ndugulile wakati akijubu swali la Mbunge wa Viti Maalum,Mwantumu Dau Haji (CCM).
Katika swali lake,Haji alidai kuna wagonjwa wa kisukari,shinikizo la damu na kansa wanapata shida kubwa ya afya.
Akijibu,Dk.Ndugulile  amewataka Watanzania kuhakikisha wanajikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kufanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki,kula mlo unaofaa,kutotumia tumbaku na kupunguza matumizi ya pombe.
ReplyForward |