27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania wakumbushwa kuenzi amani

Na Imani Nathaniel, Dar es Salaam

Jaji mstaafu Joseph Warioba amesema chaguzi za hivi karibuni zimekuwa chanzo cha kugawa watu kwenye mataifa mbalimbali duniani huku Afrika ikiongoza.

Warioba ameyasema hayo jana Desemba 14, kwenye mkutano wa Nafasi ya Viongozi wa dini katika kudumisha Amani na Maendeleo nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema kwa siku za karibuni kumekuwa na mfululizo wa machafuko kwenye nchi nyingi hasa za Afrika ambazo zimetokana na siasa hatua ambayo inachochea kuvuruga Amani.

“Tumeona kwa nchi nyingi za Afrika wakiwamo jirani zetu Kenya ambao nao wamepia kwenye makovu haya, hivi sasa kuna majirani zetu Uganda ambao nako kumeripotiwa kuuawa kwa baadhi ya watu jambo ambalo linasababisha kuondoa amani.

“Hivyo kwa kuona matukio haya yote yanayotokea kwenye nchi za wenzetu Tanzania tunatakiwa kujifunza hasa kwa upande wa Bara, kwani tunajua kuwa kwa upande wa Zanzibar tulikuwa na machafuko katika chaguzi zilizotangulia.

“Mwaka huu katika Uchaguzi wa hapa nchini maandalizi ya kupiga kura yalifanywa vizuri sana ikiwamo kuongeza idadi ya vituo vya kupigia kura na kwa mara ya wanza tume iliweka vijana ambao walikuwa wakuomba kadi yako na kukuelekeza kiasi kwamba mtu ulikuwa unatumia nusu saa tu.

“Hivyo, wananchi wanatakiwa kuwa na imani na mchakato mzima wa uchaguzi kwani kinyume na hivyo ndiyo imekuwa chanzo cha vurugu na upotevu wa amani katika nchi mbalimbali na kwamba amani ni mhimu kwenye taifa lolote,” amesema Jaji Warioba.

Kwa upande wa       Katibu wa Baraza la Maaskofu nchini, Charles Kitima, amewataka watanzania kujua maana ya amani ni kuzingatia misingi ya usawa mbele ya sharia.

“Hii yote ni pamoja na kuheshimu katiba ya nchi yetu kwani bila kuheshimu katiba hiyo tutaharibu Amani ambayo imekuwapo, hivyo tunatakiwa tujirekebisha ili tusiwe na taifa baya mbeleni,” amesema Kitima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles